Pritty Vishy adai kufanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio

Pritty Vishy amedokeza kuwa ananuia kufanyiwa sajari ya kuinua na kuongeza makalio yake ili kuwashtua maEx wake

Muhtasari

•Pritty Vish amesema kuwa nia yake ya hapo awali ya kuinua na kuongeza ukubwa wa makalio  yake bado ipo.

•Mpenzi huyo wa zamani wa stevo Simple Boy amesema kuwa atafanya hivo ili kuwashtua wapenzi wake wa zamani.

Pritty Vish
Image: Instagram

Mtayarishaji wa maudhui ya kidijitali Purity Vishenwa almaarufu Purity Vishy amefunguka kuhusu mipango yake ya kufanyiwa sajari ili kuongeza na kuinua makalio yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram,Pritty Vishy amewakumbusha mashabiki wake kuhusu mpango wake wa kufanyiwa sajari ili kuongeza ukubwa wa makalio almaarufu kama "Brazilian Butt Lift Surgery".

Hapo awali, mpenzi huyo wa zamani wa mwimbaji Stevo Simple Boy alikuwa amedokeza nia yake ya kuinua makalio yake.

Muunda maudhui huyo alionyesha kufurahia huku akidai kuwa yuko tayari kuvumilia makali ya aina yoyote ile, almradi mwili wake unapata shepu mpya na ya kupendeza ili awashtue wapenzi wake wa zamani.

"... natumai wote mnakumbuka nilipowaambia nitafanya upasuaji wa kuinua makalio mwaka huu... mpango bado unaendelea na nimefurahi sana kwa kweli ...yani nataka kushtua maex" Pritty Vishy aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Pritty Vishy ni miongoni mwa watayarishaji wa maudhui ambao wamechipuka kwa haraka sana, huku uhusiano wake wa kimapenzi na Stevo Simple Boy ukiongelewa kwa mara na mara, kabla ya wawili hao kukosana.

Baadaye, Pritty Vishy alidaiwa kujiingiza kwenye mahusiano mengine japo hakubainisha jina la mpenzi wake kutokana na sababu zake mwenyewe.

Mwishowe tena akatangaza kuachana na mpenzi wake kutokana na sababu kuwa alikuwa mtu wa kifamilia.