Bien ataja wasanii wawili kike anao wamezea mate

Mimi nina dream women, wako wengi..we tebu niambie Tems ani DM inabidi tuh niongee na wife hata ingekuwa wewe, aty Shenseea ameni DM anaeza ni Hit and Run

Muhtasari

•Tems ni msanii wa Nigeria, wakati Shenseea ni msanii wa Jamaica.

•"Sitawahi kupekua simu ya mwanamke kwa sababu naamini ndivyo unavyokufa."

Bien Aime Baraza
Bien Aime Baraza
Image: Facebook

Msanii wa Kenya Bein Aime amewataja wasanii  wawili wa kike maarufu  anao wamezea mate wakati wote.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Obinna TV, Bien alimtaja msanii wa Nigeria Tems na msanii wa dancehall wa Jamaica Shenseea kama wasanii wawili wa kike mashuhuri anao watamani wakati wote.

“Mimi nina dream women, wako wengi..we tebu niambie Tems ani DM inabidi tuh niongee na wife hata ingekuwa wewe, aty Shenseea ameni DM anaeza ni Hit and Run…..‘” Bien alishiriki.

Tems ni msanii wa Nigeria, wakati Shenseea ni msanii wa Jamaica.

Hitmaker huyo wa ‘Lifestyle’ pia alifichua sababu iliyomfanya aamue kumchagua mkewe Chiki kuwa meneja wake, akieleza sababu mbili nyuma yake, ambazo ni kwamba anaaminika na ni rahisi kumpata.

“Huo ndio uamuzi bora zaidi ambao nimewahi kufanya na inaeza kuwa sio sawa kwa watu wengine na hiyo ni juu yao kwa sababu mimi ndio navaa hiyo kiatu kwa ajili yangu, nilihitaji mtu ambaye angenisaidia kuzingatia kazi yangu, na pia nataka usimamizi ninaweza kuamini, na akuna kitu kikubwa kuliko familia kufanya kazi pamoja?

 Yeye ni meneja wangu; anasimamia kila kitu ambacho meneja wa msanii hufanya. Anapanga ratiba yangu, ziara zangu, anajadili viwango vyangu, mikakati ya jinsi tunavyosonga mwaka huu, kimsingi kila kitu ambacho meneja hufanya kwa msanii.Bien alisema.

Bien anaamini kwamba wanaume hawapaswi kufikia simu ya wapenzi wao kwa sababu huo unaweza kuwa mwisho wa maisha yao.

"Sitawahi kupekua simu ya mwanamke kwa sababu naamini ndivyo unavyokufa."

Bien pia alisema iwapo mke wake Chiki atamdanganya kwenye uhusiano, ataondoka, na hiyo itakuwa ni kwa sababu ya ubinafsi wake, na atafanya vivyo hivyo ikiwa atamdanganya.

“Kwa sababu utanisumbua bana,” Bien alisema.