Moureen Ngigi afichua kukejeliwa mtandoni kwa kujifungua kwa njia ya upasuaji

Nilikuwa nimejifungua tu, na watu walikuwa bado wanauliza kwa nini nilionekana kuwa mjamzito," alisema.

Muhtasari

•Nilijifungua kupitia upasuaji, sababu ya mimi kutaka kuzungumza na wewe kama bado hio kitu kiko ndani yangu, imenisumbua sana.

•Walikuwa wakiniambia sijui uchungu wa kuzaa ni nini. Sikupata nafasi ya kuzaa, na sijajua uchungu wa kuzaa kwa hivyo sijakua mama bado."

Moureen Ngigi na Commentator 254
Image: Instagram

Mkewe Commentator 254, Moureen Ngigi anakumbuka  changamoto alizopita baada ya kujifungua.

Anasema alinyanyaswa na kudhalilishwa mtandaoni jambo ambalo bado linamuathiri mama huyu wa mtoto mmoja, kosa lake lilikuwa tu kujifungua kwa njia ya upasuaji.

Moureen alikuwa wazi na alizungumzia uchungu wa kudhalilishwa na wanyanyasaji mtandaoni.

Alisema kwamba alikuwa na shinikizo la damu alipokuwa mjamzito.

“Nilijifungua kupitia upasuaji, sababu ya mimi kutaka kuzungumza na wewe kama bado hio kitu kiko ndani yangu, imenisumbua sana. Tulirudi nyumbani, lazima uendelee na maisha, kwa hivyo watu hawakuelewa walikuwa juu yangu sana.

Picha ya kwanza niliyopiga hospitalini, bado nilikuwa na tumbo hio,” alielezea.

"Nadhani bado sijapona na sehemu inayoumiza zaidi wanawake ndio walikuwa wananiattaack sana. Mambo ambayo wengi wao walikuwa wanasema, ‘kwani ako na ball engine?’.

"Nilikuwa nimejifungua tu, na watu walikuwa bado wanauliza kwa nini nilionekana kuwa mjamzito," alisema.

Baada ya jaribio gumu la kujifungua, Moureen alijifungua mtoto wake kwa njia ya upasuaji, kama alivyoshauriwa na daktari wake wa uzazi.

Moreen alisema anajitahidi kukuza awe na mwili munene ili kustahimili unyanyasaji kutoka kwa mtandao.

"Walikuwa wakiniambia sijui uchungu wa kuzaa ni nini. Sikupata nafasi ya kuzaa, na sijajua uchungu wa kuzaa kwa hivyo sijakua mama bado."