Ujumbe wa shukrani kutoka kwa mastaa waliopokea Jezi kutoka kwa Michael Olunga

Zawadi ya jezi hiyo iliambatana na ujumbe ulioandikwa kwa mkono kutoka kwa Olunga

Muhtasari

•Mchezaji kandanda Michael Olunga aliwashangaza watu mashuhuri kadhaa wa Kenya kwa zawadi za jezi yake.

•Baadhi ya mastaa waliopokea jezi hiyo ni pamoja na watangazaji wa redio Gidi Ogidi, Maina Kageni na Carol Radul.

•Jezi hizo ziliambatana na ujumbe, uliyoandikwa kwa mkono na Olunga, akithamini nafasi ya kila mmoja.

Gidi, King Kaka,Carol Radull wakiwa na zawadi ya jezi kutoka kwa Olunga.
Image: Instagram

Mchezaji wa kimataifa wa Kenya Michael Olunga aliwazawadi mastaa ya Kenya zawadi ya jezi yake wikendi.

Mastaa hao walijitokeza kwenye mitandao yao mbalimbali ya kijamii kuonesha zawadi waliyopokea kutoka kwa mshambuliaji huyo—jezi yake yenye namba 14.

 Pia walituma ujumbe wa shukrani kwa mchezaji huyo wa Qatar, ambaye kwa sasa yuko Malawi na timu ya taifa, Harambee Stars, wakijiandaa kwa mechi zijazo za kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Mastaa wa redio Gidi Ogidi, Maina Kageni, Carol Radul, na rapa King Kaka ni miongoni mwa waliopokea zawadi hiyo.

 Kageni, kwenye post yake kwenye akaunti yake ya Instagram, alisema;

 “Asante @ogadaolunga …kifurushi kimepokelewa vyema. Jumapili yangu imeundwa. Wewe ni shujaa wangu!!!!!!!!”

 Ujumbe sawia pia ulishirikiwa na Gidi mtangazaji wa radio jambo.

"Ni suprise ulioje, asante sana nahodha wa Harambee Stars @ogadaolunga kwa zawadi hii nzuri. Nimepata Jersey ya Ku watch nayo fainali za Champions League. Ahsante sana OLUNGA"

“Tangu siku za Gor . Mungu anatuonyesha kupitia wewe kuwa inawezekana. Endelea kututia moyo na asante kwa kit. 2nd Slide @ogadaolunga,” King Kaka alichapisha kwenye Instagram.

“Inanyenyekea sana wakati gwiji anapotambua upendo wako kwa mchezo huo mzuri. @ogadaolunga Asante! na kuendelea kung'aa na kuwatia moyo mamilioni kote Kenya, Afrika na ulimwengu. Kuwa na wiki nzuri ya familia ya mitandao ya kijamii,” alibainisha Carol Radull.

 Zawadi ya jezi hiyo iliambatana na ujumbe ulioandikwa kwa mkono kutoka kwa Olunga akielezea kuthamini mchango wa kila mtu mashuhuri katika soka la Kenya.