Manzi wa Kibera awasihi wasanii kuendesha akaunti zao wenyewe badala ya wasimamizi

Shikilia account yako na mikono yako kwa sababu akisema anakufungulia account, hizo account ndio atatumianga kukubring down.”

Muhtasari

•Mitandao ya kijamii ni chombo chenye nguvu kwa wasanii kuunganishwa kibinafsi na mashabiki wao, na kuwaamini wasimamizi na hili huenda lisiwe wazo zuri.

•Shikilia account yako na mikono yako kwa sababu akisema anakufungulia account, hizo account ndio atatumianga kukubring down.”

ndani ya studio za Radio Jambo
Manzi wa Kibera ndani ya studio za Radio Jambo
Image: RADIO JAMBO

Sosholaiti wa Kenya Manzi Wa Kibera ameeleza sababu zinazomfanya afikirie wasanii hawapaswi kuwaamini kabisa wasimamizi wao kuendesha akaunti zao.

Akiongea katika mahojiano, alikiri wazi jinsi meneja wake anavyompa wakati mgumu kwa kumkashifu kupitia kuunda akaunti ghushi kwa kutumia jina lake kwa sababu tu walitofautiana.

“Huyu manager wangu ametengeneza akunti na  jina langu ya zamani ako hadi telegram with 2,000 subscribers leo ndio amedelete picha uzuri niliscreen record niko na kila kitu nataka nimshtaki with that account as cyber bullying kwa police station, I swear to God," alisema.

Akichangia sababu za msingi kwa nini wasanii wanapaswa kudumisha udhibiti wa akaunti zao badala ya kukabidhi jukumu hili muhimu kwa mameneja wao.

Manzi Wa Kibera aliwakumbusha wasanii kuhakikisha hawawakabidhi wasimamizi wao akaunti zao za kibinafsi kwa sababu wakati fulani maishani, wanapoanguka wanaweza kutumia akaunti hizo kuharibu sifa zao.

Mitandao ya kijamii ni chombo chenye nguvu kwa wasanii kuunganishwa kibinafsi na mashabiki wao, na kuwaamini wasimamizi  huenda lisiwe wazo zuri kwa sababu ikiwa wanaharibu sifa yako, basi itakuwa vigumu hata kwa chapa kukutumia wewe kama msanii.

"Shikilia account yako na mikono yako kwa sababu akisema anakufungulia account, hizo account ndio atatumianga kukubring down," aliongezea.