Biashara zangu huniingizia pesa zaidi ya muziki wangu-Diamond

Hapo awali, lebo hiyo iliwasajili Harmonize, Rayvanny, na Rich Mavoko kabla ya kuondoka.

Muhtasari
  • Mbali na kuwa mwanamuziki, mwimbaji huyo anamiliki lebo ya muziki ambayo imewasajili Zuchu, Mbosso, Lava Lava, DVoice na Queen Darleen.
Image: INSTAGRAM// DIAMOND PLATNUMZ

Staa wa bongo kutoka Tanzania Diamond Platnumz anasema kama angekuwa anaangalia kiasi cha pesa anachoingiza kwenye tasnia ya muziki basi angeachana na muziki huo.

Mwimbaji huyo alisema alikuwa akipata pesa zaidi kutoka kwa biashara zake zingine.

"Ili ukue, lazima uwe na majukumu zaidi ambayo yataongeza pesa zaidi. La sivyo, ningetoka kwenye tasnia ya muziki," alisema.

Akiongeza, "Biashara nilizo nazo sasa zinaniingizia pesa zaidi kuliko muziki ninaofanya."

Aliendelea kushauri "Lakini hutakiwi kuondoka, unahitaji tu kuongeza kazi zaidi."

Mbali na kuwa mwanamuziki, mwimbaji huyo anamiliki lebo ya muziki ambayo imewasajili Zuchu, Mbosso, Lava Lava, DVoice na Queen Darleen.

Hapo awali, lebo hiyo iliwasajili Harmonize, Rayvanny, na Rich Mavoko kabla ya kuondoka.

Diamond pia anamiliki media house ambayo ina TV na kituo cha redio. Mwimbaji huyo pia ni balozi wa chapa kadhaa ikiwa ni pamoja na chapa ya pombe, chapa ya simu na chapa ya mawasiliano.