Mchezaji Victor Boniface ampa Ksh 130k mzee aliyerekodiwa akipiga hustle kama seremala

Katika video hiyo ambayo ilivuma mitandaoni sikiu chache zilizopita, mzee wa watu aliyeonekana kudhoofika kiafya alikuwa anahangaika kutafuta riziki akikata mbao kwa msumemo akiwa hana shati, mbavu zikionekana.

Muhtasari

• Inaweza kukumbukwa kwamba Boniface na mtengenezaji wa skit Sabinus walianzisha msako wa kumtafuta mzee huyo. Sabinus hata aliahidi kutoa N1 milioni.

Image: HIsani

Mshambuliaji wa Nigeria na klabu ya Byer Leverkusen ambao ni mabingwa wa ligi ya Ujerumani Bundesliga ameripotiwa kutoa msaada wa Naira milioni 1.5 sawa na shilingi 130k za Kenya kwa mzee mkongwe aliyerekodiwa kwenye video akihangaika na kutafuta riziki kama seremala.

Katika video hiyo ambayo ilivuma mitandaoni sikiu chache zilizopita, mzee wa watu aliyeonekana kudhoofika kiafya alikuwa anahangaika kutafuta riziki akikata mbao kwa msumemo akiwa hana shati, mbavu zikionekana.

Vide hiyo naarifiwa kumfikia mshambuliaji huyo wa Leverkusen ambaye kutokana na vidhibitisho vya jumbe za miamala, alituma hela hizo kwa ajili ya kumsaidia mzee huyo.

Mzee huyo alikua miongoni mwa gumzo lililovuma mtandaoni huku msamaria mwema akisambaza video hiyo ya kugusa moyo ambayo ilionyesha mzee huyo akihangaika wakati akiendelea na kazi yake ya useremala.

Kwa bahati nzuri, video hiyo ilisambazwa na watu wengi na watu wengi walichangia kumpatia mwanamume huyo nafasi ya kuwa na maisha bora zaidi.

Inaweza kukumbukwa kwamba Boniface na mtengenezaji wa skit Sabinus walianzisha msako wa kumtafuta mzee huyo. Sabinus hata aliahidi kutoa N1 milioni.

Hata hivyo, inaonekana Boniface, ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya Bundesliga Bayer Leverkusen alimfikia kijana aliyeshiriki video hiyo.

Alituma jumla ya N2 milioni, akiomba mzee huyo apewe milioni 1.5 na mvulana aliyeweka video hiyo anapokea N500k kwa msaada wake.

Kitendo hiki kimeyeyusha nyoyo za wengi waliompongeza kwa wema wake kwa mwanamume huyo huku risiti ya malipo ikisambazwa mtandaoni.