Mtaachana tu! Zari na Shakib wawajibu wapambe

Wanadai nimelala na wanaume wengi, lakini siwezi kutoa ushahidi.

Muhtasari

•Zari Hassan na Shakib Lutaaya walifanya mahojiano ya wazi na kujibu madai kwamba ndoa yao haitadumu, na kuwaambia wenye chuki.

•Wapenzi hao ambao waliachana hivi majuzi kabla ya kurudiana baada ya video ya Zari na mpenzi wake wa zamani, Diamond Platnumz kusambaa mitandaoni, waliwataka watu kuacha kuwahukumu wengine.

•Zari na mume wake walifunga ndoa katika harusi ya rangi na maridadi mnamo 2023 nchini Afrika Kusini.

ZARI HASSAN na Shakib Lutaaya
Image: INSTAGRAM//

Zari Hassan na mumewe, Shakib Lutaaya, wamewakemea watu wenye chuki wanaosubiri ndoa yao kuvunjika.

Hivi majuzi, wapenzi hao wenye furaha walikuwa na mazungumzo ya waziwazi ambapo walizungumza kuhusu ndoa yao.

 Kwa pamoja walikashifu watu wanaowachukia wakidai ndoa yao itaisha kwa machozi ya hali ya juu, wakiwataka watu kuacha kuhukumu maisha yao ya nyuma.

Zari Hassan na Shakib Lutaaya walifanya mahojiano ya wazi na kujibu madai kwamba ndoa yao haitadumu, na kuwaambia wenye chuki kwamba wao wako pamoja milele.

"Wanadai nimelala na wanaume wengi, lakini siwezi kutoa ushahidi. Watu hubadilika wanapokutana na mtu. Hawafanyi tena walivyokuwa wakifanya zamani," Zari alisema.

Zari na mume wake walifunga ndoa katika harusi ya kupendeza na maridadi mnamo 2023 nchini Afrika Kusini.

Harusi ya wapenzi hao ilihudhuriwa na watu mashuhuri wa Kiafrika, miongoni mwao ni rafiki wakubwa wa Zari na waigizaji kadhaa kutoka kipindi cha TV cha Young, Famous & African reality TV, marafiki wa karibu na wanafamilia.

 Hivi majuzi, katika mahojiano na vyombo vya habari vya Tanzania, mama huyo wa watoto watano alizungumzia kuhusu ndoa yake na Shakib na uhusiano wake na ex wake, Diamond Platnumz, pamoja na mambo mengine.