Vera afanya bonge la party kusherehekea kuvunjika kwa ndoa yake akisisitiza “ndoa ni utapeli”

Sidika katika mahojiano alisema kwamba jambo linalomfurahisha Zaidi na mwaka huu kuelekea kipindi cha majira ya joto ni kwamba hana mimba wala hayuko katika ndoa, hivyo atapata muda mzuri Zaidi wa kujirusha kwa raha za kila aina.

Muhtasari

• Sidika kupitia ukurasa wake wa Instagram alipakia mfululizo wa picha na video akionyesha jinsi aliwasili katika tafrija hilo kubwa aliambatanisha na ujumbe mkuu kuhusu tafrija hilo.

• “Tafrija ya kusherehekea talaka inakuja, ndoa ni utapeli,” aliandika Sidika kwenye insta story yake.

Vera Sidika.
Vera Sidika.
Image: Facebook

Mwanasosholaiti Vera Sidika amewaacha wengi katika hali ya mshangao baada ya kuandaa tafrija kubwa kwa ajili tu ya kusherehekea kuvunjika kwa ndoa yake mwezi Septemba mwaka jana.

Sidika kupitia ukurasa wake wa Instagram alipakia mfululizo wa picha na video akionyesha jinsi aliwasili katika tafrija hilo kubwa aliambatanisha na ujumbe mkuu kuhusu tafrija hilo.

Sidika ambaye alikuwa ameoleka kwa msanii Brown Mauzo kwa kipindi cha miaka 3 na kupata watoto wawili pamoja aliwataarifu mashabiki wake kwamba ameamua kuandaa bonge la tafrija kusherehekea kuvunjika kwa ndoa, akisema ndoa ni utapeli mkubwa sana kuwahi kutokea katika maisha yake.

“Tafrija ya kusherehekea talaka inakuja, ndoa ni utapeli,” aliandika Sidika kwenye insta story yake.

Mama huyo wa watoto wawili – Asia Brown na Ice Brown – alionekana akishuka kwenye gari bichi nyakati za usiku huku amezingirwa na mabaunsa na kuzindikizwa kwenye ukumbi mkuu kulikoandaliwa tafrija hiyo.

Mapema mwezi jana, Sidika katika mahojiano alisema kwamba jambo linalomfurahisha Zaidi na mwaka huu kuelekea kipindi cha majira ya joto ni kwamba hana mimba wala hayuko katika ndoa, hivyo atapata muda mzuri Zaidi wa kujirusha kwa raha za kila aina.

Alisema kwamba alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanamume raia wa Nigeria lakini akasema kuwa si uhusiano ambao anaweza sema ni ule wa kumwajibisha sana kwani yuko mguu mmoja ndani na mguu mwingine nje.

Mjasiriamali huyo alisema kwamba hatarajii kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi ambao utamfungia kwa majukumu kwani anataka muda wake wa kujirusha na pia kama ni kupata mtoto basi ni baada ya kama miaka 7 hivi ijayo, wala si wakati wowote hivi karibuni.