“Niliamua nipatie wazee muda wapumzike kidogo!” Betty Kyallo kuhusu umri wa mpenzi mpya

“Hata mpenzi wangu angekuwa 21 huyo bado ni mtu mzima, lakini umri wake si 21. Hebu tuache kuingia sana kuhusu hilo, tuliamua tuwapatie wazee muda wapumzike kidogo, unajua, wajishughulishe na mambo yao."

Muhtasari

• Kyallo pia alirejelea suala la umri wa mpenzi wake ambaye wengi wamekuwa wakizua uvumi kwamba ni kijana wa miaka 21.

•Kulingana naye, hata angekuwa mwenye umri wa miaka 21 bado huyo si mtoto kwani ameshapita umri wa miaka 18 lakini alisisitiza kwamba umri wa mpenzi wake si miaka 21.

Image: INSTAGRAM// BETTY KYALLO

Mtangazaji mpya katika runinga ya TV 47, Betty Kyallo kwa mara nyingine amezungumzia suala la maisha yake ya kimapenzi ya jinsi yanavyowapa shida watu pindi wanaposikia kuwa Betty yuko kwenye mahusiano.

Katika mahojiano ya kipekee ya Plug TV Kenya, Kyallo alisema kwamba kwa sasa hawezi kulalamika kwani yuko katika nafasi nzuri kimaisha ambapo pia anahisi kabisa kuwa anapendwa.

“Kusema kweli mimi siwezi lalamika, niko katika sehemu nzuri na pia nahisi napendwa vilivyo. Lakini mbona maisha yangu ya kimapenzi yanawatatiza watu? Mimi niko katika sehemu nzuri, nilipata mtu ambaye tumeelewana,” Kyallo alisema.

Kuhusu kipindi cha muda ambao wamekuwa wakichumbiana pamoja na mpenzi wake ambaye amekuwa akimficha kutoka kwa watu wa mitandaoni, Kyallo alisema;

“Nisingependa kutoa maelezo mengi sana kuhusu hilo kwa sababu kuna watu wa macho mabaya kule nje lakini Mungu ametulinda. Tumekuwa pamoja kwa kama miezi 8 sasa. Mimi ni mtu wa kuweka kila kitu mitandaoni lakini yeye hapendi maisha ya mitandaoni, lakini si kwamba namficha. Watu wametuona huko nje. Ukweli kwamba sijamposti haimaanishi kwamba namficha. Huwa tunaenda kila mahali kutoka migahawani, kwa supermarket na kila mahali, kwa sasa naweza sema simfichi, tunaishi tu maisha ya kawaida.”

Kyallo pia alirejelea suala la umri wa mpenzi wake ambaye wengi wamekuwa wakizua uvumi kwamba ni kijana wa miaka 21.

Kulingana naye, hata angekuwa mwenye umri wa miaka 21 bado huyo si mtoto kwani ameshapita umri wa miaka 18 lakini alisisitiza kwamba umri wa mpenzi wake si miaka 21.

“Hata mpenzi wangu angekuwa 21 huyo bado ni mtu mzima, lakini umri wake si 21. Hebu tuache kuingia sana kuhusu hilo, tuliamua tuwapatie wazee muda wapumzike kidogo, unajua, wajishughulishe na mambo yao. Kuhusu harusi sisi tuko harusi kwa sasa, hiyo stori ya harusi na kupatiwa watu presha hapana, acha tu nishughulikiwe na mtoto wa wenyewe kwa sasa,” alisema.