Mungai Eve aweka wazi uhusiano wake na Mc Gogo

“Ni rafiki yangu tu. Hatuna zaidi ya hapo.” Mungai Eve alisema.

Muhtasari

•Eve alisema yeye ni rafiki yake mkubwa, na ninaheshimu uhusiano wake na pia hatujaiangaliana kutoka kwa mtazamo huo.

•Hii inatokea baada ya fululizo wa picha walizopiga pamoja juzi na kuzua mazungumzo mtandaoni.

Mungai Eve na Mc Gogo
Image: instagram

MwanaYoutube Mkenya Mungai Eve amefafanua uhusiano wake na MC Gogo.

Akizungumza wakati wa mahojiano na Obinna TV, alifunguka, akisema kwamba haoni kama wengi wanavyodhani kuwa na yeye ni rafiki tu hakuna zaidi.

“Ni rafiki yangu tu. Hatuna zaidi ya hapo.” Mungai Eve alishiriki tukio.

Anaendelea kufafanua kwa nini hatawahi kuchumbiana na Mc Gogo akisema ni kwa sababu tayari yuko kwenye uhusiano na hataki kuchumbiana na mtu ambaye ni mdogo kwake au wa rika sawa.

"Yeye ni rafiki yangu mkubwa, na ninaheshimu uhusiano wake na pia hatujaiangaliana kutoka kwa mtazamo huo.

Hasa mimi na pia mahali ninapoketi, singependa kuchumbiana na mtu wa rika moja au ambaye ni mdogo kuliko mimi kutokana na uzoefu wa kibinafsi.” Mungai Eve alisema.

Kulingana na Mungai Eve, angechumbiana na mtu ambaye anamzidi umri wa miaka 3 hadi 4, akikiri kwamba ingemfaa.

Hii inatokea baada ya fululizo wa picha walizopiga pamoja juzi na kuzua mazungumzo mtandaoni, wengi wakidhani kwamba hatimaye Eve amepata mpenzi baada ya kuachana hivi karibuni na Trevor.

Eve pia alieleza kwa nini hawezi kumudu kuchumbiana na Obinna kama vile Obinna alivyojaribu kumuuliza, akisema sababu ni kwamba ana mizigo mingi.

“Wewe hapana, una mizigo mingi sana baby mama maigizo ya hapa na pale. Sitaki kuchukiwa hapa na pale!!” Mungai alisema.