Usijiingize kwa jambo ambalo hulijui- Ushauri wa Eve Mungai kwa vijana

Trevor alitangaza kwamba mnamo Februari 19, 2024, walikuwa wameachana, katika uhusiano na kitaaluma.

Muhtasari
  • Zaidi ya hayo, Eve alieleza kuwa anafikiri hawakuwahi kuwa na wakati wa kufurahia ujana wao walipoanza kuchumbiana Trevor alipokuwa na umri wa miaka 20 na Eve akiwa na miaka 19 pekee.
MUNGAI EVE.
MUNGAI EVE.
Image: Instagram

Mtayarishaji wa maudhui maarufu Eve Mungai aliwashauri vijana wote kuepuka kujiingiza katika jambo lolote wasilolijua linapokuja suala la mahusiano.

Alitoa ushauri huu baada ya kuulizwa kuhusu mafunzo aliyopata kutokana na uhusiano wake wa awali wa miaka 5 na Director Trevor.

Akiwa kwenye mahojiano Eve alisema;

” Nilichojifunza ni. Ningependa kuwashauri vijana huko nje kufurahia ujana wao tu. Furahia wakati huo wa kuwa mchanga, "alisema.

Zaidi ya hayo, Eve alieleza kuwa anafikiri hawakuwahi kuwa na wakati wa kufurahia ujana wao walipoanza kuchumbiana Trevor alipokuwa na umri wa miaka 20 na Eve akiwa na miaka 19 pekee.

"Nilihisi kama hatukuwahi kuwa na wakati huo wa kuwa wachanga, kwa sababu tulikutana nikiwa na umri wa miaka 19 na yeye alikuwa na umri wa miaka 20 kwa hivyo hatukujua tulichokuwa tukijiingiza," alielezea.

Hatimaye alimalizia kwa kuwaambia vijana wote wasiingie katika jambo wasilolijua.

"Singemshauri mtu yeyote ajiingize katika jambo ambalo kwa kweli hajui," alihitimisha.

Alipoulizwa amefikia wapi sasa na mafanikio aliyoyapata ni kwa sababu ya Trevor, Eve alikubali na kumpa maua yake huku akimtakia kila la kheri katika safari yake hiyo.

"Sawa, ninathamini jukumu alilocheza na ninathamini umbali tuliofikia pamoja...kwa kuwa sasa kila mtu ameenda kivyake, namtakia kila la heri," alisema.

Director Trevor amewahi kuzungumzia ripoti za kutengana kwake na Mungai Eve katika mahojiano.

Alifichua kwamba aliachana na Eve Mungai muda mrefu kabla hawajatangaza hadharani kutengana kwao, lakini walikuwa wameendeleza ushirikiano wao wa kikazi hadi Februari 2024, mambo yalipobadilika.

Trevor alitangaza kwamba mnamo Februari 19, 2024, walikuwa wameachana, katika uhusiano  na kitaaluma.