Brendah Jons aeleza kwanini aliacha kuwa “cute Christian”

“siku chache zilizopita, niliamua kuacha kuwa mkristo wa kawaida na kuwa mwenye msimamo mkali zaidi."

Muhtasari

•Kabla ya kutangaza kwamba alikuwa ameokoka na kuanzisha ukurasa mpya, mtayarishaji wa maudhui alikuwa amechukua miezi michache nje ya mitandao ya kijamii.

•Alisema kuwa ameanza kuwa serious na kuwa mkali zaidi katika mahubiri kwa kuhakikisha anafanya kile ambacho ni sahii bila kujali wale ambao hawakubaliani naye wanafikiria nini.

Brendah Jons
Image: Brendah Jons/INSTAGRAM

Muundaji wa maudhui Brendah Jons ameeleza kwa nini aliacha kuwa cute Christian au mkristo wa kawaida.

Brendah ambaye alikuwa akisambaza taarifa hio kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, alisema kuwa ameanza kuwa serious na kuwa mkali zaidi katika mahubiri kwa kuhakikisha anafanya kile ambacho ni sahii bila kujali wale ambao hawakubaliani naye wanafikiria nini, kwani hiyo ni jambo sahihi kufanya.

“siku chache zilizopita, niliamua kuacha kuwa mkristo wa kawaida na kuwa mwenye msimamo mkali zaidi. Nilisema nitahubiri ukweli, hata ukweli ambao wengi hawataki kuusikia. Nilikumbushwa sikuitwa kuwa mzuri, lakini niliitwa kuwa nuru ya ulimwengu, chumvi ya dunia.”

Brendah jons pia alikumbusha umma kwamba Mungu kamwe hawaachi watu wake, na jinsi mbio zinavyoweza kuwa ngumu, hawapaswi kamwe kuacha kumwamini mungu.

Siku fulani unaweza kujisikia kukata tamaa, mdhaifu, na kushindwa kuomba, kusoma neno, au kuabudu na ni ukweli siku hizi zipo tunapotembea na mungu.

Jambo moja ninalokumbushwa ni kwamba hata katika siku hizo, bado ninapaswa kuinuka na kuendelea kujaribu, kujikokota hadi mbele zake, na kumwambia tu jinsi siku yangu ilivyokuwa.”

Alimalizia kwa kuwauliza mashabiki wake ikiwa wanafanya hivyo, ikiwa wanafanya kila kitu kulingana na neno la bwana mamba yatakuwa sawa.

"Sijui hii ni ya nani, lakini inuka, mtoto wa mungu najua hujaomba kwa muda hujafungua Biblia yako kwa muda mrefu unaendelea kupanga mipango ya kuomba, lakini unakosa. Mungu bado anakungoja urudi mahali hapo pa maombi wewe na yeye pekee mnajua.

 Bado anasubiri wewe umsikie yuko tayari anakupenda, na anakujali. inuka mtoto wa mungu rudi kwenye upendo wa kwanza,” Brenda alisema.

kabla ya kutangaza kwamba alikuwa ameokoka na kuanzisha ukurasa mpya, mtayarishaji wa maudhui alikuwa amechukua miezi michache nje ya mitandao ya kijamii.