Dem wa facebook awashauri wanawake kuacha kulia baada ya heartbreak

"Kupata mtu mwenye nia sahihi ni ngumu. Kwa sasa nataka kufanya kazi kwa bidii na kupata pesa kwanza," alisema.

Muhtasari

•Mchekeshaji huyo alifichua kuwa hakuwa na haraka ya kuingia kwenye uhusiano, akisema kupata mtu wa kweli ni nadra.

•Dem wa Facebook aliwashauri wanawake kuwa na mpango wa kando kila wakati wanapokuwa kwenye mahusiano.

Dem wa Facebook

Dem wa Facebook amewashauri wanawake kuacha kupoteza muda kulia baada ya kuumizwa moyo na wapenzi wao.

Alitoa maoni kwamba ni rahisi kuendelea ikiwa kuna mpango wa kando kuliko kujihurumia na kulia kwa huzuni.

"Watu wakiwachwa ndio wanakuwa motivational speakers, but uki advise mtu ako in love about relationships, hawezi sikia anaona you don't want them to prosper,” alisema.

Mcheshi huyo alisema saa moja ilitosha kuingia kwenye uhusiano mwingine baada ya kuachana.

"Saa moja inatosha. Mbadilishe mara moja! Daima uwe na back up boyfriend unapokuwa kwenye uhusiano kwa sababu mambo yanaweza kubadilika.

Sometimes past paper inapitishanga mtihani. Ukiwachwa na main unaenda kwa back up," alisema.

Dem wa Facebook alikumbuka wakati aliwacha katika mahusiano na kusema tangu wakati huo ni yeye uwaacha wanaume.

"Nilichumbiana na rafiki yake wa karibu. Tangu wakati huo, sijawahi kuachwa mimi ndiye ninatupa wanaume," alisema.

Alisema yeye ni single na hayuko na haraka ya kuingia katika uhusiano.

"Kupata mtu mwenye nia sahihi ni ngumu. Kwa sasa nataka kufanya kazi kwa bidii na kupata pesa kwanza," alisema.