Obinna azungumzia maisha yake baada ya kupata mtoto akiwa na miaka 20

"Uhusiano hushindwa mara kwa mara lakini jambo moja ambalo ni la kudumu ni wazazi wakati mtoto anahusika."

Muhtasari

•Alikiri kwamba ilikuwa mojawapo ya makosa makubwa maishani, akitaja kwamba hakuwa na hekima ya kutosha kuharakisha kupata mtoto katika umri huo.

•Obinna aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni mara yake wa kwanza katika swala ya mapenzi alipopata mtoto wake wa kwanza

OGA OBINNA
Image: KWA HISANI

Mchekeshaji Oga Obinna aeleza jinsi alivyopata  mtoto wa kwanza akiwa na umri wa miaka 20.

Alikiri kwamba ilikuwa mojawapo ya makosa makubwa maishani, akitaja kwamba hakuwa na hekima ya kutosha kuharakisha kupata mtoto katika umri huo.

Katika mahojiano , alishiriki maelezo na mkufunzi wa maisha Benjamin Zulu kuhusu jinsi alivyoishia na mamake mtoto wake kwanza.

Obinna alisimulia kwamba alikuwa anatoka kijijini wakati huo, na alikuja kutafuta malisha bora  alipokutana na mama wa mtoto wake wa kwanza.

"Wakati huu nilikuwa Nairobi, nilikuwa mvulana wa mitaani, nimefanya kazi zisizo za kawaida.

 Kwa kweli nilikuwa namaliza shule yangu ya upili. Nilipokutana kwa mara ya kwanza tukaanza kuzoeana nikapata kazi ya mjumbe wa ofisi Greenworld International, nilikuwa nikilipwa Ksh 10,000. Nilihamia nyumba ya mabati ya Ksh 4,000.

 Nilikuwa naona mimi niko tayari kutulia. Kwa hivyo nikamwambia mzazi mwenzangu ambaye ni mama wa mtoto wangu wa kwanza akuje, tutulie.

“Nilikuwa najua Ksh 10,000 kutoka kijijini ni pesa nyingi sana.

Obinna aliendelea kusema kuwa ilikuwa ni uzoefu wake wa kwanza wa mapenzi alipopata mtoto wake wa kwanza.

Mimi huwaambia watu kila mara, nilipata mtoto wangu wa kwanza, nilipokuwa na umri wa miaka 20, ilikuwa uzoefu wangu wa kwanza wa mapenzi.”

 Obinna amekuwa akitumia hadithi yake kuwashauri wanaume vijana.

Mchekeshaji huyo anawashauri wanaume kuwajibika kila wanapozaa watoto na watu wanaochumbiana nao.

“Ukizaa you better take charge na pia ukiamua kushika mimba usitumie mtoto kama money Magnet for your benefit.

Uhusiano hushindwa mara kwa mara lakini jambo moja ambalo ni la kudumu ni wazazi wakati mtoto anahusika." Aliongezea.