Harmonize asifia Kiingereza chake licha ya kuishia darasa la 7 tu, “Sikufunzwa na yeyote!”

Msanii huyo alisema kuwa ujasiri wake – licha ya kutokuwa na ujuzi saana kwenye Kiingereza - ndio ambao umemfanya kujisukuma Zaidi na kukutana na baadhi ya mastaa wakubwa kutoka Marekani akiwemo Bobby Shmurda.

HARMONIZE
HARMONIZE
Image: Facebook

Bosi wa Konde Music Worldwide Rajab Kahali maarufu kama Harmonize amesifia Kiingereza chake kilichopigwa msasa Zaidi tofuati na siku za nyuma.

Akizungumza katika mazungumzo ya kipigia debe tamasha lake litakalofanyika mwishoni mwa mwezi huu, Harmonize alikiri kwamba yeye ni mtu aliyeishia elimu ya darasa la saba na hajawahi kumtafuta mwalimu yeyote wa Kiingereza kumfunza.

Msanii huyo alisema kwamba imekuwa juhudi zake kujifunza mwenyewe na kuwa na ujasiri wa kuzungumza mbele za watu, akisema kupambanya pambanya ndiko kujua.

“Unajua nikisema ujasiri ndio ambao umenifanya mimi kuwa hivi, cha ajabu Zaidi ni kwamba mimi sijawahi kwenda kwa mwalimu yeyote, sitaki kudanganya. La pili ni kwamba mimi nimeishia darasa la 7 kabisa, lakini kwa sababu nilikuwa na huo ujasiri nikasema kwamba dunia imefunguka na anaweza kuwa cochote atakaye, nikasema nitajaribu,” Harmonize alisema.

Msanii huyo alisema kuwa ujasiri wake – licha ya kutokuwa na ujuzi saana kwenye Kiingereza - ndio ambao umemfanya kujisukuma Zaidi na kukutana na baadhi ya mastaa wakubwa kutoka Marekani akiwemo Bobby Shmurda ambaye alifanikisha kolabo naye.

“Vitu ambavyo nimevipitia kwenye maisha yangu vinanifanya niamini kwamba mtu unaweza kuwa chochote utakachokuwa. Mimi sijawahi kata tamaa. Mimi ukiniuliza hapa kaitka akili yangu ninawaza kutinga katika nafasi ya kwanza kwenye Billborad, na hilo ni suala la muda tu, naamini inawezekana,” aliongeza.