Mwanamuziki Khaligraph Jones ametangaza kuwa atatoa bidhaa za bure kwa waandamanaji wa Gen Z kabla ya maandamano ya Jumanne ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, Khaligraph alichapisha kuwa bidhaa hizo za bila malipo ni kulingana na kanuni ya mavazi ya maandamano na kuwataka raia wote wanaopenda kumjulisha.
"Tuesday Dresscode, Free merchandise tunaleta Town Hit me kama Unataka #rejectfinancebill2024," aliandika.
Ishara ya mwanamuziki huyo inakuja kabla ya maandamano yanayotarajiwa kufanyika Jumanne wakati mswada huo utawasilishwa kwa usomaji wa Tatu.
Baadhi ya wanamuziki na watumbuizaji wamejitokeza kwenye mitandao yao tofauti ya kijamii kuunga mkono maandamano hayo.
Mwandishi wa maudhui Andrew Kibe pia alitangaza msimamo wake kuhusu maandamano hayo akisema ataungana na waandamanaji wa Gen Z katika kupigana mswada huo tata.
"Imekuwa hatua muhimu katika nchi yetu hivi sasa, na ninataka kuwashukuru Gen Z kwa sababu wamenifungua macho. Nilikuwa nimepotea, lakini sasa nimepatikana.
Ninataka kukuhakikishia, gen Z, na kila mtu mwingine ambaye yuko katika harakati hii, kwamba niko hapa kwa 100%.
Hata kama hamnitaki, mimi niko ndani. Wewe ni bora na mimi. Niamini, tuko vizuri pamoja,” Kibe alisema kwenye chapisho katika mtandao wake wa X.
Kibe aliahidi kushiriki kikamilifu katika maandamano hayo na kuwapongeza waandamanaji vijana kwa ujasiri wao na azma ya kupigania haki zao.
“Ndiyo maana nawapongeza Gen Z kwa sababu mmemshika ng’ombe pembe zake.
Mimi si sehemu ya mfumo huo wa serikali nipo na Gen Z. Niko ndani 100%. Nitakuwa mstari wa mbele, kama mbaya mbaya,” alisema.