logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mchungaji Ng’ang’a ahidi kushiriki maandamano siku ya Jumanne

Mchungaji Nganga alisema kuwa atakuwa katika maandamano hayo kama mwananchi wa kawaida

image
na Davis Ojiambo

Burudani24 June 2024 - 09:32

Muhtasari


  • •Alieleza kukerwa kwake na kifo kilichotokea wakati wa maandamano wiki iliyopita na kusema wanaosababisha waendelee lakini wajue kuwa kesi yao inawasubiri na ipo siku wataondoka.
  • •Mchungaji Nganga alisema kuwa atakuwa katika maandamano hayo kama mwananchi wa kawaida

Mwasilishi wa kanisa ya Neno Evangelist Mchungaji Ng’ang’a sasa amewahakikishia umma kwamba hawatatembea peke yao siku ya Jumanne, ambayo itakuwa tarehe ambapo maandamano ya pili yatafanywa kupinga Mswada wa Fedha wa 2024.

Mchungaji Ng’ang’a, ambaye alikuwa akizungumza na waumini wake kanisani, alisema kwamba atashiriki maandamano ya nchi nzima kwa sababu ya uchovu wa serikali ya sasa ya Kenya.

Alieleza kukerwa kwake na kifo kilichotokea wakati wa maandamano wiki iliyopita na kusema wanaosababisha waendelee lakini wajue kuwa kesi yao inawasubiri na ipo siku wataondoka.

Mchungaji Nganga alisema kuwa atakuwa katika maandamano hayo kama mwananchi wa kawaida.

"Hata mimi nitakuwa kwa hiyo maandamano sasa mje na teargas mnipige,ninaweza zungumza  kama mwananachi nitaacha pastor hapa wacha mtaniona tuh." Mchungaji Ng’ang’a alisema.

Mchungaji Ng’ang’a alishiriki masikitiko yake na Serikali ya Kenya Kwanza kwa kulenga ardhi yake kila mara, ambayo anadai haifai kupokonywa kutoka kwake.

“Kuna shamba yangu iko kule naivasha acre kumi na tano naskia kuna watu wa serikali wameweka fence wamechukua acre sijui acre tano na 5,000 na moja ni yangu hapo ole wako wewe.

Siku moja mtaondoka watu wenye mashamba ndio wananyayasa wale hawana nafikiri hiyo maaandamano ingine hata mimi nitakuako,” alisema.

Hii si mara yake ya kwanza kukashifu kuhusu ardhi ya kanisa lake kwamba aliarifiwa kwamba inapaswa kuhamishwa kwa sababu iko kando ya barabara.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved