MC Jessy avunja kimya baada ya shinikizo kutoka kwa mashabiki kuhusu mswada wa fedha

Mtani huyo alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri ambao walichelewa kutoa maoni yao kuhusu mswada wa fedha.

Muhtasari

•MC Jessy alisema kuwa anaunga mkono maandamano dhidi ya Mswada wa fedha wa 2024 baada ya chapisho lake refu akimjibu Khaligraph Jones.

•Maandamano yanaendelea hii leo Jumanne ,Juni 25 kwenye miji tofauti ,Kenya.

Image: INSTAGRAM//MC JESSY

Mchekeshaji MC Jessy amefunguka juu ya uamuzi wake kuhusu mazungumzo yanayoendelea kuhusu mswada wa fedha.

Shinikizo limewekwa kwa watu mashuhuri kadhaa juu ya maoni yao kuhusu mswada wa fedha.Mtani huyo alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri ambao walichelewa kutoa maoni yao kuhusu mswada wa fedha.

Hivi majuzi alimjibu mwanamuziki Khaligraph, ambaye alikuwa mdadisi kuhusu maoni yake.

"@khaligraphjones ndugu yangu, ni kweli. Niliipigia kampeni serikali hii waziwazi. Nilikuwa mstari wa mbele kusherehekea William ruto aliposhinda. Hata ushahidi wa video upo. Wakati huo, nilikuwa na matumaini sana katika utawala wake." alisema.

Alieleza kuwa alitarajia serikali kufanya kazi kama ilivyoahidi lakini hilo kwa upande wake aijatendeka.

"Nilijua ajenda yangu ya uchumi wa ubunifu itafikiwa. Waziri wetu wa Ubunifu hajafanya kile kinachohitajika. Na anajua hilo vizuri sana," aliongezea.

Alieleza kuchoshwa na mazungumzo ya ahadi na kueleza hata kama aliunga mkono serikali tawala wakati huo msimamo wake saa hii umebadilika.

"Pia nimechoka na mazungumzo na ahadi tu. Kwa hivyo hata kama 2022 niliunga mkono utawala, haimaanishi kuwa nibaki kuunga mkono maamuzi yao wakati wanatukandamiza sote. Ninaunga mkono mabadiliko tunayohitaji kama watu." Jessy alisema.

Aidha alitoa msimamo wake kuhusu mswada wa fedha akisema kwa sasa hakubaliani na mswada wa fedha.

”Ungenivotia nikue mbunge ungeuliza kama nili vote. Kwa sasa tuongee mambo ya rejectfinancebill2024.”

Hatma ya mswada huo wa fedha bado haijajulikana huku wakenya wengi wakiahidi kujitokeza katika maandamano yanayofanyika leo.