“Sihitaji kufanya DNA tena!” MP Kaluma aonyesha furaha bintiye kushiriki maandamano ya Gen Z

Kaluma alisema kuwa sasa amethibitisha uhalisia wa kuwa huyo ni mwanawe na hahitaji tena kufikiria kufanya DNA.

Mbunge wa Homa Bay Mjini Peter Kaluma ameonyesha furaha yake baada ya kumshuhudia binti yake akiwa miongoni mwa vijana wengi waliojitokeza kushiriki maandamano ya kupinga kupitishwa kwa muswada tata wa fedha 2024.

Kupitia ukurasa wake wa X, Zamani jukwaa likijulikana kama Twitter, Kaluma alipakia video ya binti yake mwenye umri wa makamo akiandamana na wenzake huku akiwa anapeperusha bendera.

Kaluma alisema kuwa sasa amethibitisha uhalisia wa kuwa huyo ni mwanawe na hahitaji tena kufikiria kufanya DNA.

“Hapa sihitaji tena kufanya DNA, binti yangu huyu,” Peter Kaluma alisema.

Awali tuliripoti kwamba mbunge huyo wa Azimio alikuwa ametoa onyo kwa wanawe wote kwamba wasipojitokeza kujiunga na wenzao katika kushiriki maandamano, atatilia shaka kuwa ni wanawe na atafikiria kufanya vipimo vya DNA.

"Mtoto wangu yeyote ambaye hataungana na watoto wengine wa Kenya mitaani Jumanne hii kupinga kutozwa ushuru kupita kiasi na ufisadi wa serikali atakabiliwa na kipimo cha DNA! Watoto wa Kenya lazima watembee pamoja ili kufaulu tulipofeli," mbunge huyo alisema.

Hii hapa video bintiye akiandamana;