Dem wa Facebook amkejeli Dr. Ofweneke baada ya kudharau umbo lake la mwili

“Aliniita miwa nikafurahi juu niko na sukari na miwainasaidia kampuni, lakini mbona akaniita miwa na yeye ni mjaneee.” Alisema.

Muhtasari

•Alimkashifu  Ofweneke, akisema yeye si mkamilifu kama anavyofikiria, kwani yuko nyuma kuwa na mwanamke maishani mwake.

•Akisema ni kwa sababu anavaa kama mzee, hivyo kuwafanya wanawake waogope kumkaribia kwa sababu wanahisi watakuwa wanamtongoza baba yao.

DEM WA FACEBOOK na DR.OFWENEKE
Image: instagram

Dem Wa Facebook alimkashifu Dkt. Ofweneke, kwa jinsi alivyoelezea umbo lake la mwili.

Dem Wa Facebook, ambaye alikuwa akizungumza  kwenye kipindi cha wiki pamoja Oga Obinna.

Alimkashifu  Ofweneke, akisema yeye si mkamilifu kama anavyofikiria, kwani yuko nyuma kuwa na mwanamke maishani mwake.

Alisema pia Ofweneke amefika  hatua ambayo anaweza kubarikiwa. au kulaani

“Dk. Ofweneke mjaneee hana bibi na hiyo old age yote alafu aliniita mimi miwa, alisema kila mtu na miwa yake…hana bibi na hiyo miaka yake saa hii ni ya kubariki wajukuu.” Dem Wa Facebook alisema.

Kwa vile hakuwa na shida kukubali majina au kauli yake  kutoka kwa Ofweneke, alijiona ni bora kuliko yeye ambaye bado hajajifanyia manufaa katika kazi yake.

“Aliniita miwa nikafurahi juu niko na sukari na miwainasaidia  kampuni, lakini mbona akaniita miwa na yeye ni mjaneee.” Alisema.

Hakuacha hipo, kwani pia alieleza sababu inayomfanya Ofweneke kuwa na bahati mbaya siku zote  linapokuja suala la mahusiano.

Akisema ni kwa sababu anavaa kama mzee, hivyo kuwafanya wanawake waogope kumkaribia kwa sababu wanahisi watakuwa wanamtongoza baba yao.

“Ofweneke hajui kupiga luku anavaa kama mzazi, madem wanaogopa kumkatia juu ya heshima ya baba.” Dem Wa Facebook alisema.

Pia alimwambia  Ofweneke akae mbali naye.