logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wale wanakuja wakisema wako na watoto wa Fred, tafadhali wafanane na Fred – Eric Omondi

Itkumbukwa Fred alifariki katika ajali ya barabarani akiwa ameabiri pikipiki wiki mbili zilizopita majira ya alfajiri.

image
na Davis Ojiambo

Burudani28 June 2024 - 14:03

Muhtasari


  • • “Wale watu wanakuja wakisema eti wako na watoto wa Fred, tafadhali, mtoto afanane na Fred,” Eric alisma huku waombolezaji wakiangua kicheko.
Eric Omondi

Eric Omondi amewachekesha waombolezaji katika ibada ya wafu ya kaka yake Fred Omondi iliyofanyika asubuhi ya Ijumaa katika makafani ya Chiromo jijini Nairobi.

Akizungumza jinsi walivyokuwa wanapendana na kaka yake, Eric alisema kuwa kaka yake siku zote alikuwa anasema kuwa angependa sana watoto wake wote wamfanane.

Eric kwa njia ya utani aliwaambia wanawake wote ambao huenda wanapangac kuibuka na madai kwamba wana watoto ambao walizaa na kaka yake Fred kuhakikisha jambo la mwanzo kabisa watoto hao wanamfanana marehemu.

“Wale watu wanakuja wakisema eti wako na watoto wa Fred, tafadhali, mtoto afanane na Fred,” Eric alisma huku waombolezaji wakiangua kicheko.

Itkumbukwa Fred alifariki katika ajali ya barabarani akiwa ameabiri pikipiki wiki mbili zilizopita majira ya alfajiri.

Katika ajali hiyo, Fred alifariki papo hapo huku dereva wa bodaboda akipelekwa hospitalini na kutangazwa kufariki siku chache baadae.

Katika hafla hiyo ya ibada ya wafu kwa ajili ya Fred, hio lilibainishwa na ikafahamika kwamba dereva huyo wa bodaboda aliyetambulika kwa jina moja tu kama Mutuku alizikwa hivi majuzi.

Omondi aliahidi kuisaidia familia yake kupitia wakfu wake wa Sisi Kwa Sisi, baada ya kumalizana na maziko ya kaka yake ambayo yanatarajiwa kufanyika Jumamosi ya Juni 29 nyumbani kwao Sega kaunti ya Siaya.

Katika ibada ya wafu iliyofanyika kwenye mochwari ya Chiromo, mastaa waliohudhuria ni pamoja na Eric Omondi, Lynne, Terence Creative, Milly Chebby, Mc Jessy, Don Nyachio, 2Mbili, Sandra Dacha, Akuku Danger, Ezra FBI, Bushka Model miongoni mwa wengine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved