Edday Nderitu amwandikia Samidoh ujumbe wa hongera baada ya kufuzu na digrii yake ya kwanza

Ujumbe huu unakuja siku chache baada ya wawili hao kuonekana katika mazingira ya kujivinjari nchini Marekani msanii huyo alipotembelea familia yake.

Muhtasari

• Ujumbe huu unakuja siku chache baada ya wawili hao kuonekana katika mazingira ya kujivinjari nchini Marekani msanii huyo alipotembelea familia yake.

Edday Nderitu, mkewe msanii wa Mugithi na afisa wa polisi Samidoh Muchoki amemwaandikia mumewe ujumbe wa kumhongera baada ya kufuzu kwa digrii yake ya kwanza.

Samidoh alikuwa mmoja wa mahafali waliofuzu kutoka chuo kikuu cha JKUAT Ijumaa.

Katika ujumbe wake wa hongera, Edday Nderitu alikumbuka jinsi mumewe alifika nyumbani na kumueleza kuhusu uamuzi wake wa kurudi darasani kuifukuzia digrii ya kwanza kabisa katika maisha yake.

Edday alifichua kwamba Samidoh alirudi shuleni baada ya kupata mtoto wao wa pili na imemchukua muda huo wote wa takribani miaka 7 kufaulisha ndoto yake.

“Uvumilivu wako na kujituma kwako kumezaa matunda, nakumbuka ulipoamua kuendelea na shahada yako, tulikuwa tumemkaribisha mtoto wetu (Mike). Asante kwa kujitolea kwako na roho yako ya kweli, nimetiwa moyo milele,” Mama huyo wa watoto watatu alisema.

Aliendelea kumpongeza kwa bidii yake ya kuhakikisha anasawazisha masuala kadhaa kwa wakati mmoja ikiwemo kuitafutia familia, kusoma, kuhudumia taifa kama polisi na wakati huo huo kuwatumbuiza mashabiki wake kama msanii.

“Ulikuwa daima kwa miguu yako & kudhani kazi za nyumbani; alimtayarisha Shirleen kwa ajili ya shule na kumwacha ulipokuwa ukienda shuleni. Hukukata tamaa licha ya changamoto nyingi. Hongera sana,” alisema.

Ujumbe huu unakuja siku chache baada ya wawili hao kuonekana katika mazingira ya kujivinjari nchini Marekani msanii huyo alipotembelea familia yake.

Itakumbukwa Edday aliondoka humu nchini na kwenda Marekani baada ya kuzozana na Samidoh kuhusu kuwa katika uhusiano mwingine na seneta Karen Nyamu.

Licha ya awali Edday kuonekana mwenye uchungu dhidi ya Samidoh baada ya kutoka kimapenzi na Karen, inaonekana amejirudi na kuamua kudumisha upendo wake kwa mumewe wa Zaidi ya miaka 15.