Mwanasosholaiti Huddah Monroe afafanua maana ya profile picture yake mpya Instagram

Mjasiriamali huyo wa bidhaa za urembo pia alieleza kwamba jicho hilo kwenye utambulisho wake linamkumbusha mara kwa mara kwamba kila anachofanya binadamu kinaangaliwa na jicho la Mungu lisilolala wala kusinzia.

Muhtasari

• Kwa muda mrefu, Huddah Monroe amekuwa akitumia picha ya rais wa kwanza na mwanzilishi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta.

Hoddah Monroe na profile pic mpya
Hoddah Monroe na profile pic mpya
Image: INSTAGram

Mwanasosholaiti wa muda mrefu Huddah Monroe amejipata kwenye kikaango cha maswali mengi kutoka kwa mashsbiki wake baada ya kubadilisha picha yake ya utambulisho kwenye Instagram na kutumia picha ya jicho.

Huddah, alilazimika kutoa ufafanuzi juu ya hilo, kutokana na baadhi ya mashabiki wake kumshinikiza kufanya hivyo wakidai kwamba picha ya jicho aliyoitumia inahusishwa na nguvu za gizani katika baadhi ya filamu za ughaibuni.

Hata hivyo, Huddah alieleza kwamba picha hiyo ni mahususi kwake kwani jicho hilo linasimama kama uangalizi kutoka kwa Mungu na pia ni jicho la utoaji.

Mjasiriamali huyo wa bidhaa za urembo pia alieleza kwamba jicho hilo kwenye utambulisho wake linamkumbusha mara kwa mara kwamba kila anachofanya binadamu kinaangaliwa na jicho la Mungu lisilolala wala kusinzia.

Aidha, Huddah Monroe alikiri kufahamu kwamba Mungu katika jumuiya ya Freemason anatambulika kama mjenzi mkuu wa Ulimwengu na vyote vilivyomo.

“Kuhusu picha yangu ya wasifu - JICHO LA UTOAJI ! JICHO LA MUNGU! Macho ya kuona yote…. 💫 Inatumika kama ukumbusho kwamba mawazo na matendo ya wanadamu daima huzingatiwa na Mungu mweza yote—ambaye anatajwa katika Masonry kama Mbuni Mkuu wa Ulimwengu……” Huddah alieleza kabla ya kufungia kipengele cha kuwezesha watu kutoa maoni yao.

Kwa muda mrefu, Huddah Monroe amekuwa akitumia picha ya rais wa kwanza na mwanzilishi wa taifa la Kenya Mzee Jomo Kenyatta.