logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanasosholaiti Corazon Kwamboka adokeza kurudi kwenye taaluma ya uwakili

"Nilitafuta mwongozo kupitia sala, nikiomba ishara ya kuniongoza kutumia ujuzi wangu kwa kuhudumia wengine," alieleza Kwamboka

image
na SAMUEL MAINA

Burudani01 July 2024 - 12:17

Muhtasari


  • •"Nilipokuwa mdogo, nilikuwa na ndoto ya kuwa wakili wa kutetea wale wasioweza kujitetea wenyewe," alisema Kwamboka.
  • •"Nia yangu iko wazi na bayana ;kutetea walio kwenye hatari, hasa kina mama wanaohitaji sauti," alitangaza Corazon.

Corazon Kwamboka, mwanasheria ambaye katika miaka ya hivi karibuni amejikita zaidi katika kuunda maudhui badala ya kufanya kazi kama wakili wa Mahakama Kuu, ametangaza mabadiliko makubwa katika maisha yake.

Akizungumza kwenye Instagram, Kwamboka aliangazia matukio ya hivi majuzi katika maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha 2024.

"Nilipokuwa mdogo, nilikuwa na ndoto ya kuwa wakili wa kutetea wale wasioweza kujitetea wenyewe," alishiriki ujumbe Kwamboka.

"Licha ya kwamba njia yangu ilinipeleka sehemu nyingine kwa wakati huo, hamu ya kufanya mambo kwa utofauti ilibaki.

Kusoma sheria kwangu kulihamasishwa na waandishi kama John Grisham, haikuwa tu ndoto yangu pekee bali pia ya wazazi wangu," aliendelea Kwamboka.

Akiendeleza cheti chake cha kufanya kazi kama wakili, Corazon alitafakari safari yake baada ya shule ya sheria, akijihisi hana uhakika jinsi ya kutumia shahada yake kwa makuzi na ufanisi.

"Nilitafuta mwongozo kupitia sala, nikiomba ishara ya kuniongoza kutumia ujuzi wangu kwa kuhudumia wengine," alieleza Kwamboka

"Hivi karibuni, katika wito wa haki baada ya vifo vya waandamanaji, nilihisi wajibu wa kurudi kwenye sheria."

"Nia yangu iko wazi na bayana ;kutetea walio kwenye hatari, hasa kina mama wanaohitaji sauti," alitangaza Corazon.

"Misheni hii mpya inachochea roho yangu. Na cheti changu cha kufanya kazi kimeboreshwa, nipo tayari kuwatetea kwa moyo wangu wote wale wanaohitaji msaada zaidi."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved