“Sikuweza kufika mbali sana kimasomo!” Mumewe Zari, Shakib Lutaaya afinguka

"Sikuweza kwenda mbali sana wakati linakuja suala la kimasomo, lakini pia nilifika mahali. Nilifika mahali ambapo ninaweza sema kwamba kama ningetaka kuingia katika siasa na kuwania wadhifa wa ubunge, ninaweza,” alisema kwa mafumbo.

Muhtasari

• Hata hivyo, alijitetea na kusema kwamba kwa kusema hivyo hana maana kwamba angependa kujitosa kwenye siasa bali ni njia moja ya kueleza kwamba angalau alifika mahali kimasomo.

Shakib ajitia moyo baada ya msukosuko kukumba penzi lake na Zari.
Shakib ajitia moyo baada ya msukosuko kukumba penzi lake na Zari.
Image: Instagram

Kwa mara ya kwanza, mumwe mwanasosholaiti Zari Hassan, Shakib Cham Lutaaya amezungumzia kuhusu maisha yake ya awali kabla ya kuja kupata umaarufu, shukrani kwa uhusiano wake na Zari.

Shakib ambaye mara nyingi si muongeaji sana, hivi majuzi alichukua hatua ya kufungua chaneli ya YouTube kwa jina ‘Shakib na Zari’ – jukwaa ambalo alisema atakuwa analitumia kuelezea mashabiki wke masuala mbalimbali wasiyoyajua kumhusu lakini pia kuwa kama ghala la kuweka picha na video zake kwa ajili ya kumbukumbu siku zijazo.

Katika kipindi cha wikendi iliyopita, Shakib aliweza kuzungumzia kiwango chake cha kielimu na kwa nini huwa anaficha sana maisha yake.

Shakib alikiri kwamba kimasomo hakuweza kuenda mbali sana, huku akisema alipitia katika shule kadhaa kabla ya kukatisha safari yake ya masomo.

“Mimi nimekulia Kawempe [mtaa duni nje kidogo ya Kampala] na wakati nilishafika umri wa baleghe niliondoka nikaenda kwingine. Wakati huo nilienda kaitka baadhi ya shule ambazo nisingependa kuzitaja kwa majina. Niko na sababu zangu zingine kwa nini sitaki kutaja shule hizo, lakini baadhi yazo ziko Kawempe, na zingine ziko Gayaza…”

“Sikuweza kumaliza elimu ya chuo kikuu; kusema kweli sikuweza kwenda mbali sana wakati linakuja suala la kimasomo, lakini pia nilifika mahali. Nilifika mahali ambapo ninaweza sema kwamba kama ningetaka kuingia katika siasa na kuwania wadhifa wa ubunge, ninaweza,” alisema kwa mafumbo.

Hata hivyo, alijitetea na kusema kwamba kwa kusema hivyo hana maana kwamba angependa kujitosa kwenye siasa bali ni njia moja ya kueleza kwamba angalau alifika mahali kimasomo.

Kuhusu eneo anakotoka, Shakib alisema kwamba katika siasa mtu pekee anayemjua ni Bobi Wine, wala hamjui mtu mwingine yeyote ikiwemo mbunge wa jimbo lake anakotoka.