Shakib akanusha vikali kuwahi kuwa 'shamba boy' wa marehemu mumewe Zari Hassan

Pia alifafanua kuhusu picha yake na marehemu Ssemwanga na kusema kuwa alikuwa mwenyekiti wa Waganda waliokuwa wanaishi Afrika Kusini,

Muhtasari

• Kupitia kipindi cha kuzungumzia maisha yake kwenye chaneli ya YouTube kwa jina Zari&ShakibTV,

Image: INSTAGRAM// ZARI HASSAN

Shakib Cham Lutaaya, mumewe mwanasosholaiti Zari Hassan kwa mara ya kwanza amezungumzia uhusiano wake na aliyekuwa mume wa Zari, marehemu Ivan Ssemwanga.

Kupitia kipindi cha kuzungumzia maisha yake kwenye chaneli ya YouTube kwa jina Zari&ShakibTV, Shakib alikanusha uvumi ambao umekuwa ukienezwa mitandaoni kwa muda mrefu sasa kuwa aliwahi kuwa kijakazi wa marehemu Ssemwanga.

Shakib alisema kwamba amekuwa akisikia uvumi huo kwa muda na hakuna ukweli wowote kwani Ssemwanga walikuja kujuana na yeye nchini Afrika Kusini.

"Ni uongo, hayo ni madam tu. Mimi sikuwahi kumfanyia kazi marehemu Ivan [Ssemwanga]. Katika maisha yangu mimi sijawahi fanya kazi kama shamba boy. Mimi ni mtu mwerevu sana na kuna vitu vingine siwezi kuvifanya," Shakib alisema.

Kuhusu picha akiwa mdogo aliyopiga na msanii Diamond na marehemu Ivan Ssemwanga,  Shakib alisema kuwa kipindi hicho alikuwa anafanya kazi katika kampuni moja Afrika Kusini ambapo Diamond alialikwa kuja kutumbuiza.

"Ni picha za kweli, sio photoshop. Ni picha zilizochukuliwa miaka kadhaa nyuma. Unajua Diamond ni celeb. Nikiwa Afrika Kusini, kuna wakati nilikuwa nafanya kazi kwa kampuni fulani na Diamond alialikwa kuja kutumbuiza kwenye kampuni yetu, nikaamua kupiga picha naye kama shabiki wake," Alisema.

"Wakati huo hata hakuwa ameanza kuchumbiana na mke wangu [Zari]" aliongeza.

Pia alifafanua kuhusu picha yake na marehemu Ssemwanga na kusema kuwa alikuwa mwenyekiti wa Waganda waliokuwa wanaishi Afrika Kusini, kwa hivyo moja kwa moja lazima angeanzisha urafiki naye.

"Niliishi Afrika Kusini kwa muda mrefu sana, na yeye [Ivan] alikuwa mwenyekiti wetu, Waganda tulioishi kule. Hivyo ni bayana kwamba mimi nikiwa Mganda na wewe ni mwenyekiti wangu, ni sharti tu niwe karibu na wewe, lazima tuzungumze." Shakib alifafanua.