Ciru Muriuki asherehekea siku ya kuzaliwa ya marehemu Charles Ouda miezi 5 baada ya kufa

Ouda alifariki akiwa na umri wa miaka 38 na miezi 5 baadae, chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi kwa mashabiki wa kazi zake za Sanaa.

Muhtasari

• Hii bila shaka ni moja ya ishara na dalili zinazoashiria jinsi Ciru alikuwa amewekeza hisia zake za mapenzi kwa Ouda kabla ya mkono bahili wa kifo kuzua utengano wao.

• Itakumbukwa katika mahojiano ya hivi majuzi, Ciru Muriuki alitaja kuwa usaidizi wa mamake umemsaidia kukabiliana na msiba wa ghafla wa mpenzi wake.

CHARLES OUDA NA CIRU MURIUKI
CHARLES OUDA NA CIRU MURIUKI
Image: HISANI

Aliyekuwa mtangazaji wa TV Ciru Muriuki ameendeleza kudumisha nadhiri ya moyoni mwake kutomsahau katu mpenzi wake, marehemu muigizaji Charles Ouda.

Hili limedhihirika kwa mara nyingine baada ya Muriuki kuwakumbusha mashabiki wake na kwamba wiki hii ni moja ya siku maalum katika maisha yake kwani ndiyo wakati marehemu Ouda alipozaliwa.

Ouda ambaye alifariki mapema mwezi Februari mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha walikuwa kwenye mapenzi na Muriuki kwa muda.

Ciru Muriuki alipeleka kwenye kurasa za mitandao ya kijamii kufahamisha ulimwengu kwamba licha ya Ouda kutangulia mbele za haki, bado atasalia kuwa mpenzi wake milele, na atazidi kumuenzi.

Alimuandikia ujumbe marehemu Ouda akimtambua kama mpenzi wake wa milele na kuisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

"Heri ya siku ya kuzaliwa, mpenzi wangu wa milele," Ciru alinukuu.

Hii bila shaka ni moja ya ishara na dalili zinazoashiria jinsi Ciru alikuwa amewekeza hisia zake za mapenzi kwa Ouda kabla ya mkono bahili wa kifo kuzua utengano wao.

Itakumbukwa katika mahojiano ya hivi majuzi, Ciru Muriuki alitaja kuwa usaidizi wa mamake umemsaidia kukabiliana na msiba wa ghafla wa mpenzi wake.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Ciru alishiriki picha yake na mamake, akimsifu kama malkia ambaye alimsaidia kupata nafasi yake katika miezi iliyofuata kifo cha mwenzi wake.

Akinukuu picha hiyo, Mshauri wa Milenia alianza kwa kukiri nguvu na uzuri wa mama yake:

“Kwa kweli mimi ni binti wa mama yangu. Ninaweza tu kutumaini kuwa nusu ya mwanamke alivyo.” Aliongeza, "Nisingeweza kumaliza miezi 4 iliyopita bila yeye ... malkia."

Ouda alifariki akiwa na umri wa miaka 38 na miezi 5 baadae, chanzo cha kifo chake hakijawekwa wazi kwa mashabiki wa kazi zake za Sanaa.