Khalif Kairo aeleza anachotamani kuhusu Cera baada ya kuachana

“Nafikiri her company kusafiri peke yako ni jambo la kuchosha sana."

Muhtasari

•Kairo alieleza kuwa kama mfanyabiashara, ana shughuli nyingi ambazo zinafanya kuwa ngumu kudumisha uhusiano.

Kairo alieleza zaidi kuwa mapenzi yake kwa Cera yalikuwa ya kweli pia  alieleza kile anachotamani kuhusu Cera.

Kairo Khalifa na aliyekuwa mpenzi wake Cera Imani
Image: Instagram

Mfanyabiashara mahiri Khalif Kairo amekiri kwamba anatamani sana mda waliokuwa nao na mpenzi wake wa zamani Cera Imani, wiki kadhaa baada ya kuachana.

Khalif Kairo alikiri katika mahojiano ya hivi majuzi  kuwa alifikiria kuwa mwenye makosa na kuharakisha kutengana.

Alisimulia zaidi kwamba Cera hakuvutiwa na pesa zake.

"Unajua sio wasichana wote wanaovutiwa na kushawishiwa na vitu hivi vya kimwili na pesa.”

“Cera alikuwa mwenye kanuni nyingi sana, unajua mimi namfahamu hivyo si mtu ambaye yuko na wewe kwa sababu ya pesa au kitu chochote. “

Pesa pia haingekuwa njia ya kutengana, "alisema.

Kairo alieleza kuwa kama mfanyabiashara, ana shughuli nyingi ambazo zinafanya kuwa ngumu kudumisha uhusiano.

"Kuna masuala ambayo yanafanya watu kuachana.Nafikiri tatizo la watu kama mimi, sisi wafanyabiashara baadhi yetu tunajishughulisha sana na biashara kiasi kwamba tunasahau kulea na kukuza uhusiano.

“Na jinsi tulivyozoea kushughulika na biashara ndivyo tunavyoshughulika na mambo mengine lakini wanawake wana hisia na wakati mwingine inakuhitaji utoke nje ya eneo lako na kujaribu kuwa na hisia kidogo ambayo wakati fulani kwa baadhi yetu inakuwa tatizo,” Alieleza.

Kairo alieleza zaidi kuwa mapenzi yake kwa Cera yalikuwa ya kweli pia  alieleza kile anachotamani kuhusu Cera.

"Ilikuwa kweli unanijua, sifanyi vitu hivyo. Sifanyi kufukuzia kwa nguvu. Nimekuwa kwenye mahusiano mengi sana, ni kwamba hawa yalikuwa hadharani sana,” alisema.

Alieleza kuwa anachotamani zaidi kutoka kwa Cera ni wakati walitumia pamoja.

“Nafikiri her company  kusafiri peke yako ni jambo la kuchosha sana."

Pia kuchumbiana na mtayarishaji wa maudhui ni jambo la kufurahisha sana, wewe ni mtu wa kupiga kamera wa kila mmoja na wanahakikisha kuwa una mambo kamili,” alieleza.