Trevor afichua kumuchia Mungai Eve karibia kila kitu baada ya kuachana, ataja sababu

“Kuwa na mwanzo mpya baada ya mahusiano kuvunjika ni mkondo muhimu katika kuponya hisia zako, makuzi ya kibinafsi, kupata mwanga wa mambo, kujijenga upya kiujasiri, kuweka mipaka..." alisema.

Muhtasari

• Trevor na Eve waliachana mwezi Februari mwaka huu baada ya kuchumbiana kwa takribani miaka 6.

• Tamko la Trevor linakuja siku chache baada ya Mungai Eve kuonekana akiwa amevaa fulana nyeupe yenye maandishi kifuani kwamba mpenzi wake wa zaman ndiye shabiki wake mkubwa.

Trevor
Trevor
Image: Instagram

Kwa mara nyingine tena, Director Trevor amejipata akiburuzwa na mashabiki wake ambao wanamtaka kuangazia Zaidi kuhusu uhusiano wake na Mungai Eve uliosambaratika mapema mwaka huu baada ya miaka 6.

Trevor alijikuta akijibu maswali mengi yanayozunguka suala hilo baada ya kukubali kufanya kipindi cha maswali na majibu na mashabiki wake kupitia mtandao wa Instagram.

Mwanzilishi na mmiliki huyo wa blogu ya KOM aliulizwa sababu iliyomfanya kuondoka katika uhusiano wake na Mungai Eve na kumuachia mrembo huyo karibia kila kitu ambacho walikuwa wamefanya pamoja, isipokuwa chaneli ya YouTube, akaunti ya Facebook na vitu vingine vidogo.

“Kusema tu ukweli sasa ningebeba sufuria?” Trevor alimjibu mmoja aliyelenga kujua kwa nini hakuondoka na chombo chochote cha ndani.

Lakini pia, alitoa ufafanuzi kwa undani kuhusu kuondoka bila kitu, akisema kwamba ni jambo zuri mtu kuanza upya baada ya uhusiano.

Kwa mujibu wa Trevor, kuanza upya na kila kitu kipya baada ya uhusiano kunampa mtu fursa nzuri ya kupona kihisia, kujijenga upya na hata kukua kifikira.

“Kuwa na mwanzo mpya baada ya mahusiano kuvunjika ni mkondo muhimu katika kuponya hisia zako, makuzi ya kibinafsi, kupata mwanga wa mambo, kujijenga upya kiujasiri, kuweka mipaka na hata kufunguka upya kwa fursa nyingine,” Trevor alifafanua.

“Hili pia litakusaidia kuondoka haraka kutoka kwa uchungu wa awali na kuzingatia katika maisha yako, kuhakikisha unapata funzo kutoka kwa jana yako na kuikumbatia kesho chanya,” aliongeza.

Trevor na Eve waliachana mwezi Februari mwaka huu baada ya kuchumbiana kwa takribani miaka 6.

Tamko la Trevor linakuja siku chache baada ya Mungai Eve kuonekana akiwa amevaa fulana nyeupe yenye maandishi kifuani kwamba mpenzi wake wa zaman ndiye shabiki wake mkubwa.

Hata hivyo, haikubainika iwapo alivaa fulana yenye ujumbe huo kimakusudi ama ni sadfa tu, na pia haikujulikana kwa mara moja ni mpenzi wa zamani yupi ujumbe huo ulikuwa unalenga, japo wengi walihisi moja kwa moja ni ujumbe ulionuiwa kumfikia Trevor.