Mwimbaji Brown Mauzo na mwanasosholaiti Kabinga Jr wametimiza mwaka mmoja tangu waanze uhusiano wao.
Wapenzi hao, ambao wamekuwa wakishiriki picha zao na kushiriki jumbe za mahaba, waliingia kwenye akaunti zao za Instagram kusherehekea hatua hiyo muhimu.
Akinukuu chini ya picha zao maridadi, Brown Mauzo aliandika,
"Happy anniversary my love@kabinga-jr ndani yako nilipata rafiki wa karibu msiri na mfuasi mwenye shukrani na aliyebarikiwa nina furaha kwa safari iliyo mbele yetu to many more my angel."
Baadaye Kabinga aliweka picha hizo hizo kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram.
Mauzo alimtambulisha Kabinga wiki kadhaa baada ya kutangaza kutengana na mwanasosholaiti Vera Sidika.
"Ninakupenda kama vile sijawahi kukupenda maishani mwangu, kwa hivyo nipende kama vile haukuwahi kupenda maishani mwako," alisema mrembo huyo.