logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Justina Syokau atangaza kupeana nguo zake Zaidi ya 1,000 kama msaada, ‘Nimenona na hazinitoshi’

“Naenda gym, pia naomba mniambie chenye naweza fanya nikapunguza juu nimekuwa nikila sana chapatti."

image
na Davis Ojiambo

Burudani09 July 2024 - 05:34

Muhtasari


  • • "Ni nguo Zaidi ya 1000,” alisema huku akichkura baadhi ya nguo na kuzionyesha akidai zingine amevaa tu mara moja.
JUSTINA SYOKAU

Msanii Justina Syokau ametangaza lengo lake la kutoa nguo zake zaidi ya elfu moja kama msaada kwa kina dada.

Kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii, Syokau alichapisha video akionyesha rundo la nguo hizo kwenye nyumba yake na kusema kwamba nia ya madhumuni ya kutaka kuzitoa kama msaada ni kwa sababu hazimtoshi.

Msanii huyo maarufu kwa kibao cha mwaka 2020 alisema kwamba katika siku za hivi karibuni, nguo zake nyingi zimekataa kumtoshea kutokana na kile alichokitaja kuwa ni kunona sana kwa kula vyakula kama chapati.

“Watu wangu nina furaha leo kwa sababu nataka kutoa kama msaada nguo zangu, kwa sababu nimekuwa mnono na mfupi. Nadhani mnaona nimenona mpaka kupita kiasi hata nguo zangu haziniingii, sipati nguo inayonitosha,” Syokau alisema.

Hata hivyo alifichua kwamba licha ya kutaka kupatiana nguo zake zenye zimekuwa ndogo kwake, ameanza mchakato wa kuhudhuria mazoezi kwenye gym huku pia akiwaomba mashabiki wake kupendekeza kile anaweza fanya ili kupunguza mwili wake.

“Naenda gym, pia naomba mniambie chenye naweza fanya nikapunguza juu nimekuwa nikila sana chapatti. Hizi nguo ni nzuri za kwenda events na dates, lakini hazinitoshi. Ni nguo Zaidi ya 1000,” alisema huku akichkura baadhi ya nguo na kuzionyesha akidai zingine amevaa tu mara moja.

Ili kuwatoa wasiwasi wenye uhitaji wa nguo hizo na ambao wanaogopa kujulikana kwamba walipatiwa nguo, Syokau aliahidi kutowataja au kuwaonyesha picha zao mitandaoni, akisema kwamba lengo lake ni kutoa kama msaada bila kutangaza ni nani ambaye amefaidika na kitendo chake cha msaada.

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved