Maoni kinzani yameibuliwa baada ya kijana mmoja mwenye mtindo wa nywele za rasta kichwani kudai kwamba alifukuzwa na mchungaji katika kanisa moja alikoajiriwa na familia ya maharusi kunasa matukio yao kwa picha na video.
Kijana huyo ambaye ana taaluma ya kunasa video na picha kwa kutumia kamera alipeleka kwenye jukwaa la TikTok na kueleza madhira yake mikononi mchungaji wa kanisa hilo ambaye alikataa asipatiwe kibali cha kuingia ili kutekeleza majukumu yake kisa mtindo wake wa nywele si wa ‘kimungu’.
Alifichua kuwa alikuwa ameajiriwa kugharamia hafla ya harusi, na ingawa alifika na dreadlocks zake na alinyimwa kuingia.
Hata hivyo, alifichua kuwa alikuwa amevalia vizuri kama alivyoarifiwa kufanya.
Aliandika …
“Niliombwa nisiingie kanisani kwa sababu ya nywele zangu . Jamani, hii ni sawa?"
Alinukuu video aliyoshiriki na maneno ...“Niliombwa kutoingia kanisani kwa sababu ya nywele zangu. Jamani, hii ni sawa?"
Jamaa huyo alieleza kwamba baada ya kufungiwa nje na hafla ya harusi tayari kuanza ndani ya kanisa na kwa kuwa alikuwa tayari amelipwa, alilazimika kumpigia simu rafiki yake mwenye nywele fupi na kumtaka kufika haraka ili kumsaidia majukumu hayo, kwani asingeweza kuharibu siku kubwa na ya muhimu kwa wateja wake kwa kukosa kunasa matukio yao ya kihistoria.
Je, ni sahihi kwa mtu kuzuiliwa kuingia katika jumba la ibada kutokana na mtindo wake wa nywele au mavazi?