“Sihitaji Saa ya bei ghali, kwa sababu ni wakati wangu!” MCA Tricky adokeza kuingia siasani 2027

Tricky ambaye ni mzaliwa wa kaunti ya Machakos hata hivyo hakudokeza zaidi kuhusu wadhifa ambao atawania na eneo la uwakilishi.

Muhtasari

• Si mara ya kwanza kwa Tricky kudokeza azma yake ya kuingia kwenye siasa. Kaitka baadhi ya machapisho yake, amekuwa pia akizungumzia kuhusu nia ya kuwa kiongozi wa watu.

• "Uongo mbili tatu na Propaganda kilo nne nishakua aKENYAN PARLIAMENTARIAN ! Oh na matusi tatu hatari …." aliandika kaitka chapisho lake la Juni 18 kwenye Facebook.

 

MCA TRICKY
MCA TRICKY
Image: FACEBOOK

Francis Munyao maarufu kwa jina lake la kisanii la MCA Tricky amedokeza kujitosa katika siasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Trickyu alichapisha rundo la picha zake akiwa amevalia nadhifu na kudokeza kwa utani kwamba hayo ni maandalizi ya mavazi rasmi ya kiongozi wa watu kuelekea uchaguzi kabla suti hazijapanda bei.

Tricky alizidi kusema kwamba hahitaji kuwa na saa ya bei ghali ili kuchaguliwa kuongoza watu, kwani wakati wake ndio umewadia.

“Kujipanga panga na Suti za 2027 mapema kabla zipande bei 😆 , I dont need an expensive Watch , coz it’s my TIME!” Tricky alisema.

Hata hivyo, mchekeshaji huyo alionekana kutumia utani na ucheshi kuchagiza suala la gumzo kuhusu saa ghali ambazo baadhi ya viongozi serikalini wameonekana nazo.

Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi na waziri wa miundombinu na barabara Murkomen ni baadhi ya viongozi ambao wamevuta nyuzi za watu kwa saa ghali ambazo wanaonekana nazo katika hafla mbalimbali.

Tricky ambaye ni mzaliwa wa kaunti ya Machakos hata hivyo hakudokeza zaidi kuhusu wadhifa ambao atawania na eneo la uwakilishi.

Si mara ya kwanza kwa Tricky kudokeza azma yake ya kuingia kwenye siasa. Kaitka baadhi ya machapisho yake, amekuwa pia akizungumzia kuhusu nia ya kuwa kiongozi wa watu.

"Uongo mbili tatu na Propaganda kilo nne nishakua aKENYAN PARLIAMENTARIAN ! Oh na matusi tatu hatari …." aliandika kaitka chapisho lake la Juni 18 kwenye Facebook.

Mwanachama huyo wa Chama cha Chokora (MCA) alipata umaarufu mwaka wa 2016 baada ya kuonekana kwa mara ya kwanza katika kipindi cha Churchill Show kilichorushwa na NTV.

Iwapo atafanikisha ndoto ya maneno yake, basi atakuwa nyongeza katika orodha ndefu ya wachekeshaji walijitosa kwenye siasa.

Baadhi ya wachekeshaji maarufu ambao wameingia kwenye siasa miaka ya hivi karibuni ni pamoja na Jalang’oo ambaye alishinda ubunge wa Lang’ata, MC Jessy ambaye alilenga kuwania ubunge wa Imenti ya Kusini katika uchaguzi uliopita wa 2022, Mbunge wa Dagoretti Kusini John Kiarie, Walter Nyambane aliyelenga kuwania urais mwaka 2022 kabla ya tume ya IEBC kumfungia nje miongoni mwa wengine.