Mwanasosholaiti Vera Sidika ameibua madai kwamba DM zake zimefurika na jumbe kutoka kwa vijana wa kiume wa Gen Z ambao wengi wao wanamuomba fursa ya penzi lake.
Hii ni baada ya Sidika kuandika kwa utani kwenye insta story yake akizungumzia tetesi za wanaume wa Gen Z kuwa mafundi hodari katika suala la mapenzi na kumalizia kwa ithibati kwamba yuko single.
“Nasikia Gen Z wanajua kuchapa hiyo kitu, ni kweli ama uongo? Na kusema ukweli mimi niko single,” Vera Sidika aliandika kwenye insta story hiyo ambayo sasa imefutika baada ya kumaliza saa 24.
Katika sasisho jingine saa kadhaa baadae, Sidika alirudi kwenye instastory yake na kusema kwa mshangao kwamba haamini macho yake maelfu ya jumbe kutoka kwa wanaume wa Gen Z kwenye DM yake ambao walikuwa wanamuomba nafasi ya kumhamisha kutoka kwenye kategoria ya kuwa single.
Hata hivyo, Sidika alisema kwamba kibarua kigumu ambacho atakuwa nacho ni kuchagua anayestahiki nafasi ya kumpenda kutoka kwa wanaume zaidi ya elfu moja wa Gen Z kwenye DM yake.
“Bado niko kwenye mshangao. DM yangu iemgeuka kuwa wazima, kusema kweli. Ni vipi mtu anaweza kumchagua mmoja kati za maelfu ya Gen Z kwenye DM, wueeh. Nimeganda kaitka kipindi cha siku mbili zimepita, ndio naendelea kupata nafuu,” Vera Sidika alisema.
Hata hivyo, mmoja alimpa suluhu kwamba afanye mkutano wa ana kwa ana na wao na kuchagua mmoja ambaye jicho lake litavutiwa naye.