Nameless aeleza tofauti kuu 3 kati yake na Redsan

"Redsan huenda gym siku saba kwa wiki, Nameless hupitia mara moja kwa mwezi,” Nameless aliandika kwenye picha hiyo ya pamoja na Redsan.

Muhtasari

• Pia alisema kwamba japo Redsan ndio yule mkali kwenye muziki wake, lakini yeye ni mkali zaidi kushinda wote.

• “Redsan ni mbaya kuliko Wengi, Nameless ni mkali kuliko kila mtu,” alijitapa.

 

REDSAN NA NAMELESS.
REDSAN NA NAMELESS.

Mkongwe wa Sanaa ya muziki ya humu nchini, Nameless amedai kwamba baadhi ya mashabiki wake kwa muda mrefu wamekuwa wakipata taabu sana kumtofautisha na msanii wa dancehall, Redsan.

Nameless alisema kwamba wengi wanashindwa kuwatofautisha kutokana na kile alidai kwamba wanakaribia kushabihiana kwa kila kitu.

Hata hivyo, alieleza sababu kuu tatu zinazowatofautisha, moja akisema yeye si mweupe sana kama Redsan na pia kusema yeye hupitia gym kwa mazoezi mara moja tu kwa mwezi wakati Redsan ni kawaida kumpata kwa gym kila siku ya wiki.

“Je, inakuwaje kwamba baadhi ya watu wanashndwa kututofautisha kusema ukweli? Redsan ni lightskin, Nameless ni DarkChocolate️, Redsan huenda gym siku saba kwa wiki, Nameless hupitia mara moja kwa mwezi,” Nameless aliandika kwenye picha hiyo ya pamoja na Redsan.

Pia alisema kwamba japo Redsan ndio yule mkali kwenye muziki wake, lakini yeye ni mkali zaidi kushinda wote.

“Redsan ni mbaya kuliko Wengi, Nameless ni mkali kuliko kila mtu,” alijitapa.

Wasanii hao wawili wamekuwa kama nembo ya muziki wa Kenya kwa miaka mingi, Redsan akibadilisha jinsi watu walikuwa wanaona mziki wa dancehall humu nchini naye Nameless akijibidiisha katika muziki wa kizazi kipya.