Stevo Simple Boy afichua kwa nini anampendelea Vera Sidika kuliko Amber Ray

"Mimi na Vera ni biashara tu. Siwezi mhukumu juu sijamjua vizuri. Yule nikipatiwa siwezi m’handle, ni biashara tu,” Stevo alisema.

Muhtasari

• Akizungumzia uchu wake wa mapenzi, Stevo alisema alanega kuoa mwanamke ambaye hatakuwa anahaha kupata umaarufu.

STEVO SIMPLE BOY.
STEVO SIMPLE BOY.
Image: HISANI

Rapa Stevo Simple Boy amefunguka mrembo anayempendelea baina ya mtangazaji Betty Kyallo na wanasosholati Vera Sidika na Amber Ray.

Akizungumza kaitka runinga ya TV47, Simple Boy alisema kwamba ana ukaribu na Betty Kyallo na anaupigia saluti utu wake, tangu walipokutana miezi kadhaa iliyopita kwa chakula cha tafrija.

Akizungumzia uchu wake wa mapenzi, Stevo alisema alanega kuoa mwanamke ambaye hatakuwa anahaha kupata umaarufu.

“Mimi venye nilikuwa nimesema ya kwamba nikipata yule msichana mwenye ako serious na ndoa, mwenye hatahitaji umaarufu, huyo ndiye nitamuoa. Kuhusu Betty [Kyallo], sisi tuko pamoja na nilichovutiwa nacho kwake, ako na roho safi, ni mnyenyekevu, ni mrembo ambaye anaelewa,” Stevo Simple Boy alisema.

Alipoulizwa kuhusu Amber Ray, Stevo alisema kwamba hajafikia viwango vyake na kumsifia mwenzake, Vera Sidika ambaye alifichua kuwa na mazungumzo naye mara kwa mara, japo akasisitiza ni mazungumzo ya kibiashara tu.

“Amber Ray bado, hajatosha. Vera ndio ako na ngongingo, lakini bado… juzi nilimtext kwenye WhatsApp, ako sawa tunaongea tu. Mimi na Vera ni biashara tu. Siwezi mhukumu juu sijamjua vizuri. Yule nikipatiwa siwezi m’handle, ni biashara tu,” Stevo alisema.