Felicity Shiru aeleza hamu ya kutaka kuolewa na harusi na Thee Pluto

"Anataka tufunge ndoa ya Kiislamu. Lakini ninamwambia, nataka harusi ya kanisa. Tumekwama tu hapo.”

Muhtasari

•Shiru alishiriki kwamba mume wake anataka wafanye harusi ya Kiislamu tofauti na mapenzi yake.

•Felicity Shiru alielezea kuwa anatazamia zaidi kuolewa kwa harusi kanisani akisema siku moja itafanyika lakini ajui ni lini.

Felicity Shiru na mpenzi wake Thee Pluto

MwanaYouTube maarufu Thee Pluto bado hajafunga ndoa rasmi na mpenzi wake Felicity Shiru.

Licha ya wapenzi hao kuwa miongoni mwa watu wanaofuatwa kwa malengo yao ya kuvutia ya wanandoa, bado ajakuwa na harusi ambayo imewaunganisha pamoja.

Akiongea katika  mahojiano na Mungai Eve, Felicity Shiru alifichua kuwa ni mojawapo ya matakwa yake kuwa na harusi na The Pluto Kanisani.

Hata hivyo, mumewe Thee Pluto alijitenga na kuwa mwislamu; jambo ambalo linamfanya kutanguliza aina ya harusi ya Kiislamu.

Shiru alishiriki kwamba mume wake anataka wafanye harusi ya Kiislamu tofauti na hisia zake.

 “Kwa kawaida tunashirikiana na Pluto kuhusu hilo. Unajua sasa yeye ni Muislamu, mimi ni Mkristo."

“Kwa hiyo huwa ananiambia, anataka tufunge ndoa ya Kiislamu. Lakini ninamwambia, nataka harusi ya kanisa. Tumekwama tu hapo.”

Felicity Shiru alielezea kuwa anatazamia zaidi kuolewa kwa harusi kanisani akisema siku moja itafanyika lakini ajui ni lini.

 "Ningependa kufanya hivo. Nina hakika itatokea siku moja. Sijui ni lini,” alijibu.

Wapenzi hao wawili wamekuwa na uhusiano wenye misukosuko kwa miaka mingi.

 Thee Pluto na mpenzi wake, Felicity Shiru, wamejaliwa na binti yao mrembo, Zoey.