Malkia wa miziki ya kizazi kipya kutoka humu nchini, Nadia Mukami amevunja kimya kuhusu watu kumsema vibaya kisa muonekano wake haswa paji la uso.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Nadia Mukami alichapisha picha akionesha kwa ukaribu muonekano wa paji lake la uso na kufunguka kwamba yeye si mgeni kwa baadhi ya jumbe kwenye upande wa kutoa maoni, watu wakizua utani hasi kuhusu paji lake la uso.
Akiwajibu kwa njia ya utani, mama huyo wa mtoto mmoja alisema kwamba ukubwa wa paji lake la uso unaashiria wingi wa vitu ambavyo vimo ndani mwa kichwa chake.
Mshindi huyo wa tuzo ya AFRIMMA kitengo cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki alisema kwamba ukubwa wa paji lake la uso ni stoo yenye imehifadhi vitu vingi.
“Wakenya forehead yangu iliwafanyia nini? Hii imebeba storage ya vitu mingi,” Mukami alisema huku akimalizia na emoji ya kucheka.
Kwa muda mrefu, wanawake wengi wamekuwa wakiona aibu muonekano wa paji lao la uso, kiasi kwamba wengi wameazimia kuzama katika matumizi ya mawigi ili kuficha kina cha paji la nyuso zao.
Je, ni hatia mwanamke kuwa na paji kubwa la uso?