Dorea Chege afichua kuachana na DJ Dibul kwa wiki 2

"Nilipack vitu zangu na kuondoka kwa karibu wiki mbili. I was feeling myself. I am not saying sorry," alisema.

Muhtasari

•Dorea alikumbuka wakati alipoachana na Dibul kwa wiki mbili kwa sababu hakuweza kuomba msamaha au kutaka kuzungumza.

•DJ Dibul pia alibainisha kuwa uzoefu huo uliwafanya kutafuta njia bora za kutatua masuala yao.

Dorea Chege na Dj Dibul
Image: INSTAGRAM// DOREA CHEGE

Mwigizaji maarufu Dorea Chege amekumbuka kuondoka kwa ndoa yake kwa sababu ya ugomvi na mume wake, DJ Dibul.

Pia, katika siku za hivi majuzi, wamesemekana waliachana lakini baadaye walibatilisha madai hayo machafu kwa picha za kuadhimisha kumbukumbu zao.

Hata hivyo, katika mahojiano na Size 8 na DJ Mo kwenye kipindi chao, Dorea alifichua jinsi alivyotoka katika ndoa yao baada ya kutoelewana.

"Nilipack vitu zangu na kuondoka kwa karibu wiki mbili. I was feeling myself. I am not saying sorry," alisema.

Katika utetezi wake, Dibul alibainisha jinsi ego ina jukumu kubwa katika kuathiri mahusiano, na watu wangependelea kuondoka kuliko kujinyenyekeza.

“Wakati watu wanapendana hawawezi kukaa bila kuonana,wanafake it tu na kujifanya wako sawa, lakini ndani kabisa, wanaumia. Kuanzia hapo, hatujawahi kufika mahali hapo tena, hata tunapogombana, hatujawahi kufikia hatua hiyo."

Dorea pia alibainisha jinsi kuwa na Dibul kulifungua mawazo yake kuhusu ndoa na yale ambayo amejifunza.

"Ndoa si mafanikio ni kutafuta ndoa yenye itakuwa sawa, sasa hayo ni mafanikio," aliongeza.