Mwanasosholaiti Vera Sidika kwa mara nyingine amerejelea suala lake la kuzungumzia mapenzi na vijana wa Gen Z.
Kupitia instastory yake, Sidika amewakumbusha vijana hao wa Gen Z ambao alisema wengi walimtumia jumbe nyingi DM kutaka fursa ya penzi, akisema kwamba hajasahau suala lao, ila tu ni kwa sababu yuko mbali na nyumbani.
Mama huyo wa watoto wawili aliwapa hakikisho kwamba atakaporudi nchini Kenya, atarejelea suala hilo na ataendelea kutoka aliko achia – ambako ni kufanya chaguo kutoka kwa maelfu ya jumbe za vijana wa Gen Z kwenye DM.
“Kusema ukweli sijasahau stori ya Gen Z. Ni ile tu niko mbali sana na nyumbani. Uhusiano wa mbali hauwezi kwangu, wakati nitakapotua Kenya, tutaendelea kutoka tulikoachia,” Sidika alisema.
Wiko moj iliyopita, Sidika alifichua vijana wa Gen Z kujaza DM zake baada ya kutoa kidokezo cha kuwasifia kuwa ni mafundi hodari katika mapenzi.
“Nasikia Gen Z wanajua kuchapa hiyo kitu, ni kweli ama uongo? Na kusema ukweli mimi niko single,” Vera Sidika aliandika kwenye insta story.
“Bado niko kwenye mshangao. DM yangu iemgeuka kuwa wazima, kusema kweli. Ni vipi mtu anaweza kumchagua mmoja kati za maelfu ya Gen Z kwenye DM, wueeh. Nimeganda kaitka kipindi cha siku mbili zimepita, ndio naendelea kupata nafuu,” Vera Sidika alisema baada ya kupata jumbe nyingi DM.