logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DJ Mo: Kabla nimuoe Size 8, nyumba yangu ilikuwa na kasufuri na kaTV tu!

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa zaidi ya miaka 10 na wamebarikiwa na watoto wawili.

image
na Davis Ojiambo

Burudani21 July 2024 - 10:44

Muhtasari


  • • Mo, kwa upande wake alieleza kwamba kando na kukua kimwili, pia nyumba yae imepata vitu ambavyo asingefikiria kuwa navyo akiwa bila mpenzi.

Mcheza santuri wa muda mrefu wa nyimbo za injili, DJ Mo amefunguka jinsi ndoa ilibadilisha maisha yake na kuyaboresha.

Akizungumza katika kipindi cha Love in the Wild ambacho kinaongozwa naye na mkewe Size 8 kwenye runinga ya TV47, Mo alifichua kwamba ndoa ilimfungua macho pakubwa, jambo ambalo pengine asingelipitia kama mseja.

Mo alikuwa anajibu swali na mkewe Size 8 ambaye aliuliza kila mtu wakiwemo wageni wao, Dj Dubul na mpenziwe Dorea Chege, akiwataka kila mmoja kueleza jinsi ndoa au uhusiano ulibadilisha maisha yake.

Mo, kwa upande wake alieleza kwamba kando na kukua kimwili, pia nyumba yae imepata vitu ambavyo asingefikiria kuwa navyo akiwa bila mpenzi.

Mo aliwashangaza watu akiungama kwamba licha ya kuwa na gari kipindi hicho, lakini nyumba yake ilikuwa ina vitu vichache sana, akikumbuka kuwa vitu vya maana alivyokuwa navyo nyumbani ni sufuria na runinga tu.

“Tangu nikupate, kando na kukua kimwili, pia mimi ni mtu ambaye sasa amejipanga sawasawa. Unajua mimi nilikuwa tu na gari lakini nyumba yangu haikuwa na kitu chochote. Kulikuwa tu na kasufuria na karuninga, hivyo ndivyo vitu tu vilikuwa, unajua mradi tu niko na gari niko sawa,” Dj Mo alisema.

Kando na kufunguka akili ya kumiliki vitu, Mo pia alisema ujio wa Size 8 katika maisha yake ulimfungua akili ya jinsi ya kuwa na nidhamu ya kifedha.

“Pia makuzi ya maisha, unagundua kwamba sasa hivi pesa ziko hivi, tufanyie hiki na kile, tujenge, huwezi haribu pesa na hiki, lakini pia nimekua kiasi kwamba mimi ni baba sasa. Kusema ukweli nimekuwa mtu tofauti sana,” aliongeza.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa zaidi ya miaka 10 na wamebarikiwa na watoto wawili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved