'Sipendi venye sielewi kizungu ya Kasmuel McOure' Nasra Yusuff asema akidai kurejea shuleni

Nasra aliacha chuo kikuu mwaka wa 2018 baada ya kupata umaarufu kwenye churchil show

Muhtasari

•Mchekeshaji Nasra Yusuff ameeleza kuwa anatarajia kurudi shuleni ifikapo Septemba mwaka huu.

•Nasra anadai kuwa kurudi shuleni kutamwondolea aibu mbali mbali.

Nasra Yusuff
Nasra Yusuff
Image: INSTAGRAM

Mchekeshaji  Nasra Yusuff amesema kuwa yupo tayari kurejea darasani baada ya kuacha chuo kikuu mwaka wa 2018.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram,Nasra alisema kuwa anajutia kuacha masomo kwa kuwa alidhani elimu haikuwa na maana baada ya kuanza uchekeshaji na kupata umaarufu. 

"Majuto yangu makubwa maishani ni kuacha chuo kikuu mwaka wa 2018 baada ya kuonekana kwenye churchil show.Nilidhani elimu haikuwa na muhimu tena." Maandishi kwenye ukurasa wa Instagram yalisomeka.

Nasra ni miongoni mwa wachekeshaji ambao wamekuwa wakiwaburudisha mashabiki wa kipindi maalum kwenye runinga ya NTV ,Churchil Show.

Hata  hivyo,mchekeshaji huyo alidai kukumbushwa wakati wa kusajili wanafunzi wapya kwenye vyuo vikuu ifikapo Septemba.

"Naomba intake ya Sept mnikumbushe nirudi shule." Nsara aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Nasra alisema kuwa alikuwa akisomea kuhusu ushauri wa kisaikolojia enzi zile ila sasa amebadili mawazo yake na ataenda kusomea sayansi ya siasa hasa baada ya ongezeko la karo.

"Kozi niliyokuwa nafanya ilikuwa na gharama ya Ksh.45,000 kwa kila muhula.Nilipojaribu kujiandikisha tena siku chache zilizopita,sasa ni ksh.100,000 kwa kila muhula."

Nasra  aliongeza kwa kusema kuwa kuenda shule kutamwondelea aibu wakati wa kuwashauri watoto ambao anapanga kuwalea.

"Nkiadopt wale watoto wangu sitaki nikiwaambia masomo ni muhimu waniangalie na bombastic side eye."

Siku chache zilizopita Nasra alidai kuwa amejaribu kutafuta taarifa zozote za kusaidia kuhusu 'kuadaopt' watoto nchini Kenya bila mafanikio mengi.

Aliendelea kuwaomba mashabiki wake watoe taarifa zozote zinazoweza kumsaidia katika mchakato huo.

"Je, ni utaratibu gani wa 'kuadopt' watoto nchini Kenya. Nataka malaika wawili  ( watoto wawili) nyumbani kwangu kwa haraka."