Msanii Benson Muia almaarufu Bensoul amesema kwamba hajawahi kujutia kuacha chuo kikuu.
Kwenye mazungumzo na kituo cha spm buzz ,Bensoul anadai kuwa aliacha shule akiwa mwaka wa tatu na kusema kuwa alikuwa akisomea uhandisi.Bensoul anaamini kuwa shule ilikuwa ikichukua muda wake mwingi ambao anahisi ungekuwa wa manufaa zaidi kujikita kwenye muziki.
"Nilikuwa mwanafunzi mwerevu sana.Sababu ya mimi kuacha shule ni kwa sababu sikuwa na furaha licha ya kwamba nilipita mtihani wangu...nilihsi kuwa nilikuwa napoteza masaa mengi ambayo nilipaswa kuyatumia kwa muziki.Niliamua kuacha yote na kujikita kwenye muziki,uhandisiwa sauti na ningeweza kuchanganya nyimbo zangu mwenyewe..." Bensoul alisema.
Hata hivyo msanii huyo alisema kuwa haikuwa rahisi pindi alipoacha shule waama changamoto kama vile kukosa kulipa kodi ya nyumba zilimwandama japo anafurahia kukutana na kikosi cha Heart The Band.
"Haukuwa mchakato rahisi,nilipoacha shule...japo nafurahia kuzungukwa na marafiki wema kutoka Heart The Band."
Bensoul aliongeza kwa kusema kuwa kikosi kizima cha Heart The Band hakikuwa kikienda shule.
Msanii huyo amekuwa kipenzi wa Kenya, ametoa vibao vingi ambavyo vimemuweka kwenye ramani na kutazamwa zaidi ya milioni 1 kwenye YouTube.