Director Trevor ametetea kauli yake aliyotoa kuhusu watayarishaji wa maudhui ya kidijitali hasa wa kike wanaounda maudhui ya ngono kwa ajili yakupata umaarufu.
Trevor ameeleza kwamba ujumbe huo haukumhusu mpenzi wake wa zamani,Mungai Eve.Aliongeza kwa kusema kuwa hana nia ya kumzungumzia akidai kuwa mrembo huyo amemzuia kwenye mitandao yake yote ya kijamii na haiwezekani kuona aina ya maudhui anayounda.
"Mungai Eve ni mmoja tu kati ya watayarishaji wengi tulionao Kenya,kwa hivyo siwezi kukaa hivi niseme ana'sexualise' maudhui.Kuna wengi sana.Si vibaya kuunda maudhui ya ngono. Kama yeye ni mmoja wao hata sijui." Trevor alisema.
Hata hivyo aliendelea kwa kusema Mungai Eve amem'block' kila mahali.
"Siwezi kuona maudhui yake,amenizuia kwa hivyo siwezi kuandika kitu kinachomhusu na huwa sioni maudhui yake," Trevor alielezea.
Hapo awali,Trevor,Kupitia chapisho kwenye ukurasa wake wa Instagram aliwashtumu waunda maudhui ya kidijitali hasa wanawake ambao wanaunda maudhui ya ngono kwenye mitandao ya kijamii ili kupata umaarufu.
Hata hivyo,mpenzi wa zamani wa Trevor,Mungai Eve hakusita kumjibu Director Trevor.Kupitia mahojiano na wanahabari wa mitandao ya kijamii Eve alisema kuwa kila mtu ana uhuru wa kufanya kile anataka.
"Everybody is entitled to do what makes them happy..life is too short." Mungai Eve alisema. Alipoulizwa ikiwa anam'miss Trevor alidai kuwa hio ilipitwa na wakati na yeye si mtu wa kurejelea mambo ambayo yalipita.
"Tunaongelea mambo yatakayofanyika baadaye,si mambo yaliyopitwa na wakati.Tulikuwa kwenye mahusiano nzuri wakati ule ,ila kwa sasa kila mtu aendelee na maisha yake." Mungai Eve alisema.