Happy Birthday! Mtangazaji Massawe Japanni asherehekea siku ya kuzaliwa jijini London

Malkia huyo wa Swahili Radio ambaye kwa sasa anafurahia likizo yake nchini Uingereza anasherehekea kutimiza miaka 42.

Muhtasari

•Huku akisherehekea, mtangazaji huyo mahiri mwenye sauti ya kusisimua amemshukuru Mungu kwa kumfanya aone mwaka mwingine.

•Massawe aliendelea kusisitiza kwamba umri ni suala la akili, akibainisha kwamba ikiwa mtu hajali, basi haijalishi.

Image: INSTAGRAM// MASSAWE JAPANNI

Mtangazaji wa Radio Jambo, Massawe Japanni anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa leo, Julai 27.

Malkia huyo wa Swahili Radio ambaye kwa sasa anafurahia likizo yake ya siku ya kuzaliwa nchini Uingereza anasherehekea kutimiza miaka 42.

Wakati akisherehekea hatua hiyo kubwa, mtangazaji huyo mahiri mwenye sauti ya kusisimua alimshukuru Mungu kwa kumfanya aone mwaka mwingine.

“EST 1982, ninashukuru kuona mwaka mwingine. Mungu amekuwa mwaminifu kiajabu,” alisema Massawe kupitia mtandao wa Instagram.

Massawe aliendelea kusisitiza kwamba umri ni suala la akili, akibainisha kwamba ikiwa mtu hajali, basi haijalishi.

Mtangazaji huyo wa kipindi cha Bustani la Massawe kwenye Radio Jambo kwa sasa anafurahia likizo yake jijini London, Uingereza.

Siku ya Ijumaa, alifichua kwamba alitembelea Ikulu ya Buckingham, mahali pa kuishi kwa familia ya kifalme ya Uingereza.

"Kabla ya siku ya kuzaliwa .. natumia siku yangu katika ikulu," alisema.

Watu wengi, wakiwemo wafanyakazi wenzake wa Radio Jambo na watu wengine mashuhuri wamejitokeza kumsherehekea Massawe wakati akisherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Msomaji wa habari Valentine Ludiema ambaye amekuwa akiendesha kipindi chake cha mchana wakati hayupo alisema, “Kheri njema ya kuzaliwa.. @massawejapanni cheers, mbele kuko sawa.”

Msimamizi wa majukwaa ya mitandao ya kijamii ya Radio Jambo, Naom Nyaboke, alibainisha kuwa ni zawadi kubwa na neema kuona mtangazaji huyo bora wa redio akitimiza mwaka mmoja zaidi.

"Siku ya kuzaliwa ya leo iwe mwanzo wa mwaka uliojaa ndoto zinazotimia, malengo yaliyofikiwa, afya njema, utajiri, furaha na maisha marefu, ndio matakwa yangu ya msingi kwako," Naom alisema.

Tazama jumbe zingine kutoka kwa baadhi ya watu wengine kwa Massawe:

Zainabuzeddy: Happy birthday gal.

Kenzomatata: Happy birthday.

Nadia_mukami: Happy birthday.

Isaiahlangat: Happy birthday my sister, be blessed.

Esther.musila: Happy birthday to you wamusyi.

Sandra_dacha: Happy birthday jaber.

Nanaowiti: Happy birthday my darling.

Chriskirwa: Happy birthday @massawejapanni