YouTuber Mungai Eve kwa mara nyingine tena amezungumzia kuhusu kile alichkitaja kuwa ni swali linaloulizwa kwa wingi na mashabiki wake kuhusu ni lini anapanga kuitwa mama.
Kupitia kipindi cha maswali na majibu katika YouTube channel yake, Mungai Eve alisema kwamba amekuwa akiulizwa swali hilo kwa wingi na kufunguka kwamba kwa sasa licha ya kwamba ana ndoto za kuitwa mama siku moja lakini bado anahisi yeye bado ni mtoto.
“Mimi nahisi kwamba bado ni mtoto. Sijui lakini nahisi kwamba kila msichana ana ndoto ya kuwa mama wakati mmoja, na kusema kweli mimi binafsi huwa najiona nikiwa na familia na watoto lakini kwa sasa siko katika nafasi nzuri ya kujua ni lini, nahisi kama Mungu ndiye ana jawabu la ni lini, naweza sema miaka 3, 10 lakini Mungu anajua vizuri zaidi, mimi sijui ni lini,” Eve alisema.
Kuhusu kutumia mbinu za kupanga uzazi, Mungai Eve alisema kwamba hajaanza leo bali amekuwa akipanga uzazi tangu mwaka 2020.
“Chenye naweza sema ni kwamba kwa muda wote nimekuwa na implant tangu nafikiri 2020 na sababu niliiweka ni ya kawaida tu kwamba siko tayari kupata watoto,” aliongeza huku akisema kwamba kwake mpango huo umekuwa ukifanya kazi vizuri.
Mungai Eve pia alidokeza kuhusu uhusiano mpya wa kimapenzi, miezi kadhaa baada ya kauchana na aliyekuwa mpenzi wake, Director Trevor.
Alisema kwamba wengi waliyafahamu maisha yake ya kimapenzi kutokana na kwamba waliyaanika mitandaoni hadharani, lakini akasema kuwa ni jambo ambalo hatarajii kulirudia tena katika uhusiano mpya.