Msanii wa injili na mchungaji Size 8 amejiandikia ujumbe maridhawa wa shukrani anaposherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Size 8 alishukuru Mungu kwa kila sekunde ya uhai na afya bora licha ya pandashuka za maisha.
“Leo nasherehekea siku yangu ya kuzaliwa Mungu ni mwaminifu...... kwa wengi, kuwa na maisha sio baraka bali kwangu nathamini kila sekunde ya maisha na afya njema kwa kifo imekuwa ikitaka kunichukua lakini Mungu alinijalia. Nimeshinda magonjwa na kifo kwa hivyo ninashukuru milele kwa maisha kwa sababu ni baraka...” Size 8 alisema.
Mama huyo wa watoto wawili ambaye hivi majuzi ametangaza kuanza safari ya maisha bila mume alisema kwamba anajua safari hiyo inaonekana kuwa ngumu na mbaya lakini akaonyesha Imani yake kwamba mkono wa Mungu utamuongoza.
“Baba Mungu nalibariki jina lako takatifu asante kwa mwaka huu mpya kabisa.....na maisha yangu yanabadilika na najua hata safari hii mpya ikionekana kuwa ngumu mkono wako unaongoza njia.....ni imani yangu iko kwa wewe....”
Ni alfajiri njema, mwanzo mpya sifa ziwe kwa Mungu muweza wa yote katika jina la Yesu Kristo ambaye amehifadhi maisha yangu akiwapa wanangu zawadi ya mama woi utukufu kwa Mungu nashukuru sana...haleluya.....” aliongeza.
Mwishoni mwa wiki jana, Size 8 alitangaza kuachana na mumewe Dj Mo katika kile ambacho hakijajulikana wazi chanzo chake nini.