Nana Owiti: “Nimekuwa mdogo na najipenda nilivyo, achene kuni’DM kuhusu uzani wangu”

“Nimekuwa mdogo, na pia ninapenda jinsi nilivyo muache kuni’DM kuhusu uzani wangu wa mwili,” Nana Owiti aliandika.

Muhtasari

• “Nimekuwa mdogo, na pia ninapenda jinsi nilivyo muache kuni’DM kuhusu uzani wangu wa mwili,” Nana Owiti aliandika.

NANA OWITI
NANA OWITI
Image: FACEBOOK

Mkewe rapa King Kaka, Nana Owiti amewakomesha wanaofurika katika faragha zake wakionyesha wasiwasi wao kuhusu hali yake ya kungua kwa uzani wa mwili wake.

Kupitia instastory yake, Nana Owiti alisema kwamba anafahamu fika kwamba amekuwa mdogo kinyume na siku za nyuma na kukiri kwamba anapenda jinsi alivyo kwa sasa huku akiwataka wanaoingia kwenye DM kumuuliza kuhusu hilo kukoma.

“Nimekuwa mdogo, na pia ninapenda jinsi nilivyo muache kuni’DM kuhusu uzani wangu wa mwili,” Nana Owiti aliandika.

Owiti alichapisha video akicheza densi na marafiki zake na kutania kwamba alikuwa akifikiri kwamba ni yeye tu hajui kucheza densi hadi pale alipokutana na wenzake.

“Kwa kweli nilifkikiri ni mimi tu ambaye singeweza kucheza densi kujinasua katika matatizo, hapa ni kama nimekutana na wenzangu,” alisema.

NANA OWITI
NANA OWITI

Mama huyo wa watoto wawili shabiki sugu wa Arsenal amekuwa akipokea jumbe za mashabiki wake ambao wanaonesha mashaka yao kuhusu mabadiliko yake ya muonekano wake.

Hata hivyo, sasa ameweka wazi kwamba si jambo la kumshangaza kwani anafahamu fika kwamba amekuwa mdogo katika siku za hivi karibuni, na kuwataka wanaoingia DM kudhihirisha mashaka yao kumhusu kukoma.