Komasava: Diamond aingia kwenye charts za Billboard ya USA na kushika nafasi ya 39

Siku 12 zilizopita, waliachialia remix ya wimbo huo wakismhirikisha Jason Derulo na tayari wimbo umetazamwa mara milioni 7.8 kwenye YouTube.

Muhtasari

• Diamond alitoa wimbo huo miezi minne iliyopita akiwashirikisha Chley na Khalil Harisson ambao mpaka sasa umetazamwa mara milioni 4.8 kwenye YouTube.

• Siku 12 zilizopita, waliachialia remix ya wimbo huo wakismhirikisha Jason Derulo na tayari wimbo umetazamwa mara milioni 7.8 kwenye YouTube.

Jason Derulo na Diamond Platnumz
Image: HISANI

Msanii namba moja kutoka Afrika Mashariki, Diamond Platnumz kwa mara nyingine amepiga hatua kwenye muziki wake kwa kuingia kwenye chati za muziki za Billboard nchini Marekani kwa mara ya kwanza, shukrani kwa wimbo wake wa Komasava.

Msanii huyo aliorodheshwa katika nafasi ya 39 kwenye chati za Billboard, siku chache baada ya kushirikiana katika remix ya kibao hicho na mkali kutoka Kanada, Jason Derulo.

Ngoma hiyo ilifanikiwa kuingia kwenye kipengele cha ngoma za Afrobeats kwenye jukwaa hilo kubwa la Marekani la kuonesha mafanikio ya ngoma za wasanii mbalimbali.

Kwenye orodha ya Billboard, huwa wanaorodhesha ngoma 50 za Afrobeat ambazo zimefanya vizuri na Diamond alishika nafasi ya 39.

Kigezo kikuu ambacho Billboard wanaangalia ili kufaulisha ngoma ya msanii kwenye jukwaa lao ni jinsi wimbo umekuwa ukifanya kwenye majukwaa ya kutiririsha miziki, idadi ya vipakuliwa, mauzo bila kusahau jinsi wimbo huo umepokelewa na wakaazi wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi duniani.

Diamond alichapisha taarifa hizi na kutoa rai kwa mashabiki wake kuupeleka wimbo huo kaitka nafasi ya kwanza kwenye chati hizo za Billboard.

“Acha tupeleke huu wimbo nambari moja watu wangu,” Diamond alirai.

Diamond alitoa wimbo huo miezi minne iliyopita akiwashirikisha Chley na Khalil Harisson ambao mpaka sasa umetazamwa mara milioni 4.8 kwenye YouTube.

Siku 12 zilizopita, waliachialia remix ya wimbo huo wakismhirikisha Jason Derulo na tayari wimbo umetazamwa mara milioni 7.8 kwenye YouTube.